IQNA

Waislamu India

Vitendo vya chuki dhidi ya Waislamu vyashadidi India baada ya hekalu la Wahindu kuzinduliwa katika ardhi ya Msikiti

19:53 - January 26, 2024
Habari ID: 3478256
IQNA-Kama ilivyokuwa ikitarajiwa, baada ya kuzinduliwa hekalu la Ram, ambalo lilijengwa na Wahindu wenye itikadi kali katika sehemu ambayo zamani palikuwa na msikiti wa Babri katika jimbo la Uttar Pradesh, duru mpya ya mashinikizo ya kijamii dhidi ya Waislamu wa India imeanza.

Uharibifu wa maduka ya Waislamu katika mji wa Mumbai kwa kisingizio cha kuzuia barabara na ujenzi usioidhinishwa ni matokeo ya haraka zaidi ya ufunguzi wa hekalu la Ram. Kiasi kwamba, matingatinga yalienda mara moja kwenye Barabara ya Mira huko Mumbai ambapo Waislamu walikuwa wakipinga kufunguliwa kwa Hekalu la Ram na ujenzi wake badala ya Msikiti wa Babri.

Soroush Amiri, mtaalamu wa masuala ya bara Hindi anasema kuhusiana na suala hili: Hatua zinazochukuliwa na Wahindu wenye misimamo mikali dhidi ya Waislamu nchini India ni za kisiasa kabisa na zinafanywa kwa idhini na baraka kamili za serikali ya Kihindu ya Waziri Mkuu Narendra Modi. Katika kipindi cha utawala wake, katika jimbo la Gujarat, Wahindu wenye itikadi kali walipata fursa ya kufanya uhalifu mwingi dhidi ya Waislamu kwa lengo la kuwafukuza wafuasi wa Uislamu, na sasa uwepo wake na chama cha BJP katika serikali kuu kumewahimiza na kuwapa kichwa zaidi Wahindu cha kuwakandamiza Waislamu zaidi.

Ukweli ni kwamba chama tawala cha Kihindu cha India "Bharatiya Janata" kiliingia madarakani kikiwa na kauli mbiu ya utaifa wa Kihindu na kuimarisha misingi ya Uhindu nchini India. Kwa hakika kaulimbiu ya chama hiki ni kuwawekea vikwazo na mibinyo wafuasi wa dini za walio wachache hasa Waislamu na kuwafukuza katika ardhi yao ya asili.

Hapana shaka kuwa, Waislamu ambao ni zaidi ya watu milioni 250 katika jamii ya India yenye utitiri wa kaumu na dini, kwa maana halisi hawachukuliwi kuwa ni jamii ndogo na iliyo ya wachache kwani Waislamu wanapatikana katika maeneo yote ya India. Baba wa nyuklia wa nchi hiyo pia alikuwa Mwislamu na jamii ya Waislamu wa India ilikuwa na mchango na nafasi muhimu katika maendeleo ya nchi hiyo, lakini chama cha BJP kinaendesha mashinikizo dhidi ya Waislamu nchini India kikifuatilia malengo kadhaa na kimekuwa kikipuuza waziwazi vitendo vya kikatili vya Wahindu wenye misimamo ya kufurutu ada kuhusiana dhidi ya Waislamu.

3486957

Habari zinazohusiana
Kishikizo: india waislamu bjp wahindu
captcha