IQNA

Waislamu India

Wahindu wamuua Mwislamu Mlemavu kwa kula chakula katika hekalu India

18:42 - September 29, 2023
Habari ID: 3477669
NEW DELHI (IQNA) - Wahindu wenye msimamo mkali walimpiga na kumuuai Mwislamu mlemavu kwa kula prasad kwenye hekalu.

Prasad ni sadaka ambacho kutolewa kwa miungu ya Kihindu, ambayo kwa kawaida hujumuisha chakula ambacho baadaye hugawanywa miongoni mwa Wahindu.

Kisa hicho kilitokea katika mji wa  New Delhi katika eneo la Sundar Nagari siku ya Jumanne na polisi wamewazuilia watu kadhaa kuhusiana na tukio hilo, ripoti ya India Today ilisema.

Video ya tukio hilo inazunguka kwenye mitandao ya kijamii ambapo kundi la watu linaonekana kumpiga bila huruma mtu ambaye alikuwa amefungwa kwenye nguzo huku akiomba msaada.

Kwa mujibu wa polisi, mwathiriwa alitambuliwa kama Muhammed Israr, 26,  na kwa mujibu wa uchunguzi wa awali, alikuwa na matatizo ya kiakili kutokana na kutoweza kutoa majibu ya kuridhisha wakati genge la Wahindu lilipomhoji.

Babake mwathiriwa Abdul Wajid amewasilisha malalamishi ambapo alitaja kuwa aliupata mwili wa mwanawe nje ya nyumba yake.

Alisema kundi la watu lilimpiga mwanawe kwa fimbo kwa tuhuma za kuiba.

Majirani wa Muhammed Israr walimrudisha nyumbani baada ya kushambuliwa na kumwambia baba yake kuhusu tukio hilo lakini aliaga dunia kutokana na majeraha aliyoyapata.

Tangu Waziri Mkuu Narendra Modi aingie madarakani mwaka wa 2014, India imeshuhudia milipuko mingi ya ghasia kati ya Wahindu walio wengi na Waislamu wake walio wachache India ambao idadi yao ni zaidi ya milioni 200.

Wakosoaji wanakishutumu chama tawala cha utaifa wa Kihindu,  Bharatiya Janata (BJP) kwa kuchochea ubaguzi dhidi Waislamu tangu kuingia mamlakani.

3485350

Habari zinazohusiana
Kishikizo: waislamu india bjp wahindu
captcha