IQNA

Chuki dhidi ya Waislamu India

Mwislamu auawa India kwa tuhuma za kubeba nyama ya ng'ombe

21:28 - March 10, 2023
Habari ID: 3476686
TEHRAN (IQNA) - Mwanamume mmoja Mwislamu mwenye umri wa miaka 56 aliripotiwa kuuawa na genge la watu wenye chuki siku ya Jumatano kwa tuhuma kwamba alikuwa amebeba nyama ya ng'ombe katika jimbo la Bihar nchini India.

Naseem Qureshi, mkazi wa kijiji cha Hasanpur katika wilaya ya Saran ya jimbo hilo, alikuwa akisafiri na mpwa wake Firoz Qureshi kukutana na baadhi ya marafiki waliponaswa na kundi la watu katika kijiji cha Jogia, karibu kilomita 110 kutoka Patna.

Kulingana na polisi, wakati Firoz Qureshi alifanikiwa kutoroka, mjomba wake alipigwa kwa fimbo za mbao.

Firoz Qureshi anasema  kiongozi wa kijiji hicho Sushil Singh pia alikuwa sehemu ya umati uliotekeleza mauaji hayo..

"Walisimamisha pikipiki yetu na Sushil Singh alidai kuwa tulikuwa na nyama ya ng'ombe na kuwaamuru watu hao watupige," alisema, kulingana na ripoti hiyo. "Nilitoroka kwa njia fulani kwa kuwashinda wanaume walionifukuza."

Polisi walisema kundi hilo lenyewe lilimkabidhi Naseem Qureshi kwa polisi, na baada ya hapo alikimbizwa katika hospitali ya Siwan lakini alifariki wakati wa matibabu siku ya Jumatano.

Watu watatu - Ravi Sah, Ujwal Sharma na Singh - wamekamatwa kuhusiana na kesi hiyo, huku wengine wawili wakitoroka, kulingana na NDTV.

"Tunaichukulia kama kisa cha kushambulia watu," Msimamizi wa Polisi wa Saran Gaurav Mangla amesema na kuongeza kuwa,  "Inachunguzwa iwapo Naseem alikuwa amebeba nyama ya ng'ombe au la wakati wa tukio."

Wakati huo huo, kaka yake Naseem Qureshi, Ashraf Qureshi, alishutumu polisi kwa kuwalinda waliohusika katika ukatili huo.

Mauaji kama hayo kwa jina la ulinzi wa ng'ombe ni jambo la kawaida sana nchini India. Katika miaka michache iliyopita, nchi hiyo imeshuhudia mauaji ya kikatili kwa jina la ulinzi wa ng'ombe. Mauaji hayo yanatekelezwa na wahindi wenye misimamo mikali wa mrengo wa kulia. Ni Wahindi wachache sana wamefikishwa kizimbani baada ya jinai dhidi ya Waislamu

Kuchinja ng'ombe – ambao ni watakatifu kwa Wahindu - ni kinyume cha sheria katika baadhi ya majimbo ya India.

3482754

Kishikizo: india waislamu wahindu
captcha