IQNA

Qur'ani Tukufu

Ndugu 7 wa familia moja Misri wahifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu

19:05 - December 30, 2023
Habari ID: 3478116
IQNA - Ndugu saba katika familia ya Misri wameweza kujifunza Qur'ani Tukufu kikamilifu.

Ndugu hao saba wamefanikisha hili kwa usaidizi na kutiwa moyo na wazazi wao.

Watatu kati yao, Saad Muhammad, Saeid na Abdul Aziz walishinda tuzo ya kwanza katika kitengo cha familia ya Qur'ani Tukufu katika Mashindano ya 30 ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Misri wiki iliyopita, kwa mujibu wa tovuti ya habari ya Al-Watan.

Saad Muhammad aliiambia tovuti hiyo kwamba wazazi wake, ambao wana elimu ya shule ya msingi pekee, walikuwa na shauku ya kuona mafanikio ya watoto wao kwenye njia ya kuhifadhi Quran.

"Kaka na dada zangu na mimi sote tumesoma katika Chuo cha Kiislamu cha Al-Azhar na pia tumeweza kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu.," alisema.

Saad Muhammad pia alisema familia yake imekuwa na furaha kubwa kushinda taji la juu katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani.

Alimuomba Mwenyezi Mungu amsaidie kuwalea watoto wake katika njia ambayo wao pia watafuata njia ya Qur'ani Tukufu.

Hafidh huyo wa Qur'ani Tukufu  pia aliipongeza Wizara ya Wakfu ya Misri  kwa kuandaa tukio la kimataifa la Qur'ani.

Duru ya 30 ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Misri ilifanyika katika Kituo cha Dar-ul-Quran cha Masjid Misr,  katika mji mkuu mpya wa utawala wa nchi hiyo, kuanzia tarehe 23 hadi 26 Disemba.

Wawakilishi wa nchi 64 walishindana katika mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu.

3486607

Habari zinazohusiana
captcha