IQNA

Mashindano ya Qur'ani Tukufu

Washiriki kutoka Nchi 60 kushiriki Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Misri

22:25 - December 13, 2023
Habari ID: 3478031
IQNA - Waziri wa Wakfu Misri amesema mashindano ya kimataifa ya Qur'ani yatafanyika nchini humo kwa kushirikisha wasomaji na wahifadhi wa Qur'ani Tukufu kutoka nchi 60.

Sheikh Mohamed Mukhtar Gomaa alisema katika mkutano na waandishi wa habari kwamba washiriki 63 kutoka nchi 54, zikiwemo 20 za Afrika, 20 za Asia na 5 za Amerika na Ulaya, wamethibitisha ushiriki wao.

Idadi ya washiriki inatarajiwa kufikia 100, afisa huyo aliongeza, Misri al-Yawm iliripoti.

Kituo cha Dar-ul-Quran cha Masjid Misr katika mji mkuu mpya wa utawala wa Misri kitaandaa hafla hiyo, ambayo itakuwa ni toleo la 30 la mashindano hayo, alibainisha.

Sheikh Gomaa amesema kando ya mashindano hayo, mpango wa usomaji wa Hadithi 40 za Mtume Mtukufu Muhammad (SAW) utafanyika katika Msikiti wa Imam Hussein (AS) mjini Cairo.

Hapo awali alisema jumla ya zawadi za fedha taslimu za toleo hili zitakuwa zaidi ya pauni milioni 8 za Misri, na hilo linaashiria ukuaji wa asilimia 300 ikilinganishwa na toleo la mwaka jana.

Mashindano hayo yatafanyika katika makundi sita, ikiwa ni pamoja na kuhifadhi Qur'ani nzima pamoja na kisomo na tafsiri, kuhifadhi Qur'ani kwa wasiozungumza Kiarabu, na kuhifadhi Qur'ani kwa maimamu wa misikiti wahubiri, alisema mwezi uliopita.

Pia kuna kategoria ya kuhifadhi Quran pamoja na ufahamu wa dhana zake kwa familia, aliendelea kusema.

Habari zinazohusiana
captcha