IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Maqari kutoka nchi kadhaa washiriki 'Khatm ya Qur'ani Tukufu' nchini Misri

17:20 - December 26, 2023
Habari ID: 3478098
IQNA – Programu ya kila wiki ya Khatm Qur'an (kusoma Qur'ani Tukufu kuanzia mwanzo hadi mwisho) ilifanyika nchini Misri kwa kushirikisha maqari kutoka nchi mbalimbali.

Wasomaji wa kigeni wanaoshiriki katika hafla hiyo ya Qur'ani ni washindani katika mashindano ya 30 ya kimataifa ya Qur'ani ya Misri, yaliyoanza wiki iliyopita.

Maqari wakuu wa Misri kama Ahmed Ahmed Nuaina, Taha Numani, Ahmed Tamim al-Maraghi, Mohamed Fathallah Bibris, Yusuf Qassim Halawah, Fathi Khalif, na Mahmoud Ali Hassan pia walihudhuria prorgam ya Qur'ani ya Khatm.

Katika hotuba yake, Waziri wa Wakfu wa Misri Sheikh Mohamed Mukhtar Gomaa alisisitiza haja ya kufanya juhudi ili Qur'ani Tukufu isomwe kila mahali na kila nyumba.

Makala ya 30 ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Misri yalianza Jumamosi, Desemba 23, kwa kushirikisha wasomaji na wahifadhi wa Qur'ani kutoka nchi 64.

Kituo cha Dar-ul-Quran cha Masjid Misr katika mji mkuu mpya wa utawala wa Misri ndicho kitakuwa mwenyeji wa hafla hiyo.

 

Habari zinazohusiana
captcha