Katika mkutano wake na, Hannanah Khalfi mwenye umri wa miaka minane na aliyehifadhi kikamilifu Qur'ani Tukufu, Rais Rouhani alibainisha furaha yake kutokana na uwezo wa msichana huyo. Rais Rouhani alisema ni jambo la fahari kuona familia zenye watoto wanaofungamana na Qur'ani Tukufu nchini. Huku akiitaja familia kama hiyo kuwa ni kigezo, Rais Rouhani ametoa wito wa kuimarishwa uenezwaji wa utamaduni wa Qur'ani nchini. Huku akimpongeza msichana huyo aliyehifadhi Qur'ani Tukufu, Rais Rouhani amesema: "Msichana huyu mwenye umri wa miaka minane anasoma Qur'ani kwa lahni nzuri huku akizingatia kanuni za tajwidi."
Katika mkutano huo Rais Rouhani ameitunuku zawadi ya gari familia ya msichana huyo ambaye pia ana ndugu zake wengine watatu waliohifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu. Katika miaka ya hivi karibuni nchini Iran kumeongezeka idadi ya watoto wenye umri wa chini ambao wamehifadhi
Qur'ani Tukufu.../mh