IQNA

Jinai za Israel

Idadi ya misikiti ya Gaza iliyoharibiwa katika mashambulio ya Israel yazidi 50

13:25 - November 02, 2023
Habari ID: 3477827
AL-QUDS (IQNA) - Idadi ya misikiti iliyoharibiwa kabisa katika mashambulizi yanayoendelea ya utawala haramu wa Israel kwenye Ukanda wa Gaza imefikia 52.

Haya ni kwa mujibu wa ofisi ya vyombo vya habari vya serikali katika eneo lililozingirwa, ambayo ilisema Jumatano kwamba mashambulizi hayo pia yamesababisha uharibifu wa viwango tofauti kwa misikiti mingine 110.

Salama Marouf, mkuu wa ofisi ya vyombo vya habari vya serikali, aliambia vyombo vya habari kuwa hadi sasa wanafunzi 2,510 wameuawa katika mzozo unaoendelea.

Alisema mzozo huo umegeuza Ukanda wa Gaza kuwa "eneo la maafa, na zaidi ya watu milioni 1.5 wamelazimika kuyahama makazi yao, wakitafuta hifadhi katika makazi."

Marouf alisema kuwa wanajeshi wa Israel pia wameharibu ofisi 82 za serikali na makumi ya taasisi za huduma na vifaa vya umma.

"Shule 212 zilipata uharibifu wa viwango tofauti kutokana na mashambulizi, na shule 45 hazikuwa na huduma," aliongeza.

Jeshi la utawala haramu wa Israel limepanua mashambulizi yake ya angani na ardhini kwenye Ukanda wa Gaza, ambao umekuwa chini ya mashambulizi ya anga tangu operesheni ya kushtukiza iliyoanzishwa na harakati ya upinzani ya Hamas mnamo Oktoba 7.

Takriban Wapalestina 9,000 wameuawa katika mashambulizi ya Israel. Aghalabu ya waliouawa ni wanawake na watoto.

Kando na idadi kubwa ya majeruhi na kufurushwa, vifaa vya kimsingi vinapungua kwa wakaazi milioni 2.3 huko Gaza kutokana na mzingiro wa Israel.

3485848

Habari zinazohusiana
captcha