IQNA

Kadhia ya Palestina

Kuhani: Wazayuni hawawakilishi Wayahudi, wanataka 'Kufuta' Wapalestina

20:26 - October 27, 2023
Habari ID: 3477793
LONDON (IQNA) - Wazayuni hawawakilishi Uyahudi na wanataka "kuwaangamiza" watu wa Palestina, kuhani mwenye makao yake nchini Uingereza anasema huku kukiwa na mashambulizi ya Utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza yakiwa yamesababisha vifo vya zaidi ya Wapalestina 7,000 wengi wakiwa ni wanawake, watoto na wazee.

Haya yamesemwa na Kuhani Ahron Cohen, msemaji wa kundi la Neturei Karta nchini Uingereza, katika mahojiano na Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA)

Matamshi hayo yanajiri katika hali ya vita vikali ambavyo  utawala katili wa Israel umekuwa ukiendesha dhidi ya Ukanda wa Gaza tangu tarehe 7 Oktoba, baada ya makundi ya wapigania ukombozi wa  Palestina yenye makao yake makuu Gaza kufanya Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa, mashambulizi ya kushtukiza katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu, ili kukabiliana na utawala wa Israel ambao umezidisha jinai dhidi ya watu wa Palestina.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Palestina, mashambulizi ya Israel hadi sasa yameua zaidi ya Wapalestina 7,000, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, huku zaidi ya watu 15,000 wakijeruhiwa.

Haya hapa mahojiano hayo.

IQNA: Tunashuhudia kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel unaua raia wa Palestina huku ukidai kuwa unajilinda. Unafikiri ni kwa nini ukatili huu haujakumbana na hatua kali za kimataifa kama inavyotarajiwa.?

Cohen: Katika kipindi cha miaka 120 hivi hivi Wazayuni wamefanikiwa sana na propaganda zao katika kuushawishi ulimwengu ( wa Mayahudi na wasio Mayahudi) kwamba wanawakilisha Watu wa Kiyahudi. Kwa hivyo, hatua yoyote inayochukuliwa na ulimwengu kwa ujumla ambayo sio ya kupendeza kwa Wazayuni, inachukuliwa kuwa chuki dhidi ya Uyahudi. Tangu Vita vya Pili vya Dunia ulimwengu wa Magharibi unaogopa kutajwa kuwa chuki dhidi ya Wayahudi na Wazayuni wanatumia hofu hii kwa manufaa yao yote.

Ukweli ni kwamba, Wazayuni hawawakilishi Mayahudi. Uzayuni na Uyahudi ni dhana mbili zinazohitilafiana na zinazokinzana na hazipaswi kuchanganywa. Cha kusikitisha ni kwamba tuko mbali na hili kueleweka na kukubalika na ulimwengu kwa ujumla.

Na hii ndio sababu jamii ya kimataifa haichukui hatua za maana dhidi ya Israel.

IQNA: Unadhani ni kwa nini utawala wa Kizayuni wa Israel unatumia vibaya masuala ya kidini na kwa kisingizio cha kuwaunga mkono Mayahudi huwaua raia wa Palestina?

Cohen: Hayo yote hapo juu ni sehemu ya malengo ya Wazayuni ya kuwateka na kuwaangamiza kabisa watu wa Palestina.

IQNA: Kwa nini taasisi za haki za binadamu bado ni waangalizi tu wa jinai za Israel huko Gaza?

Cohen: Hawana chaguo lingine la vitendo chini ya hali ya sasa.

IQNA: Nini mtazamo wa Mayahudi nchini Uingereza kuhusu jinai za utawala wa Kizayuni?

Cohen: Kwa masikitiko, kuna maoni tofauti kati ya Wayahudi kuhusu Wazayuni. Kwa hivyo, jibu la swali lako litategemea ni ‘kambi’ gani alipo Yahudi. Yeyote aliye wa ‘kambi’ ya Kizayuni ataidhinisha matendo ya Wazayuni. Yeyote asiye sehemu ya ‘kambi’ ya Wazayuni atayakosoa vikali vitendo hivyo.

IQNA: Unadhani ni ipi njia bora ya kumaliza mivutano hii?

Cohen: Njia pekee ya kumaliza mivutano kwa wakati huu itakuwa ni makubaliano ya ulimwengu kwa uvunjwaji kamili wa amani wa Dola la Kizayuni la Israel na nafasi yake kuchukuliwa na taifa la kidemokrasia kwa wakaaji wote wa Palestina, wawe Wayahudi, Waarabu au mtu mwingine yeyote. Hilo lilifanyika mivutano itakoma mara moja. La kusikitisha ni kuwa tuko mbali na uwezekano wa kufikia suluhu kwa njia hii. Lakini kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu tunaweza kufikia wakati wowote kile ambacho kinaweza kuonekana kuwa haiwezekani. Kama ilivyotokea kwa mfano katika Afrika Kusini na Urusi ya Kikomunisti.

Mahojiano yamefanya na Mohammad Hassan Goodarzi

Maoni na mitazamo katika mahojiano haya ni ya mhojiwa pekee na si lazima yawe yanaakisi mitazamo ya Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA)

Habari zinazohusiana
captcha