IQNA

Kimbunga cha Al Aqsa

India yaunga mkono jinai za Wazayuni dhidi ya watu wa Gaza, wanachuo waandamana

11:41 - October 26, 2023
Habari ID: 3477790
TEHRAN (IQNA)- Katika hali ambayo, serikali ya India imechukua mkono wa sera za kuunga mkono jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza, mamia ya wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali vya New Delhi, mji mkuu wa nchi hiyo wameandamana na kulaani jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya wakazi wa Gaza.

Polisi waliwazuia wanafunzi waliokuwa wakiandamana kukaribia ubalozi wa Israel mjini New Delhi. Waandamanaji hao wakiwa wamebeba mabango na maberamu wametoa mwito wa kukomeshwa mauaji ya Wazayuni dhidi ya raia na kurejeshwa Wapalestina ardhi yao ya asili.

Sambamba na kulaani jinai za hivi karibuni zinazofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina waishio Gaza, matabaka tofauti ya wananchi wa India yamefanya maandamano katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo na kutaka kukomeshwa jinai za utawala huo dhidi ya wananchi wa Gaza. Hii ni katika hali ambayo, serikali ya India imeendelea kuunga mkono dhahir shahir jinai za Wazayuni dhidi ya watu wa Gaza na kivitendo imekengeuka sera za huko nyuma za New Delhi katika fremu ya Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote (NAM).

Zamani India iliunga mkono Palestina

Murtadha Husseini, mweledi na mchambuzi wa masuala ya kisiasa anasema kuhusiana na hili:

Huko nyuma, uungaji mkono wa India kwa malengo ya wananchi wa Palestina ulikuwa ukifahamika ulimwenguni, haswa katika ulimwengu wa Kiislamu. Lakini kwa kuingia madarakani serikali ya Wahindu ya Waziri Mkuu Narendra Modi, New Delhi imechukua mkondo wa sera za kuwa pamoja na Wazayuni katika kuwakandamiza watu wa Gaza, jambo ambalo sio tu linaharibu pakubwa nafasi ya India miongoni mwa Waislamu wa nchi hii, bali pia katika ulimwengu wa Kiislamu.

Wakati serikali ya India imewapa kisogo watu wa Gaza, kuna ripoti za masingasinga wanaoishi Marekani  kufanya maandamano mbele ya ubalozi wa India, ambapo wameitaka serikali ya Marekani  imshinikize Narendra Modi, Waziri Mkuu wa India ili akomeshe jinai dhidi ya masingasinga. Baada ya Kanada kumfukuza mwanadiplomasia wa India anayetuhumiwa kumuua mfuasi wa Sikh anayeishi Kanada, India imewafukuza zaidi ya wanadiplomasia arobaini wa Kanada.

India imemfukuza mwanadiplomasia wa Canada ikilipiza kisasi kwa hatua ya Canada kumfukuza mwanadiplomasia wa nchi hiyo. Hii ina maana kwamba, kiwango cha mvutano wa kisiasa na kidiplomasia katika uhusiano wa India na Canada kimeongezeka.

Kitendo cha India cha kumfukuza mwanadiplomasia wa Canada kinaonyesha kuwa, New Delhi haikubaliani na shutuma za Ottawa kwamba India ilihusika katika mauaji ya kiongozi wa Wasikh wanaotaka kujitenga nchini humo.  Serikali ya Canada bado inasisitiza kuwa, India ilihusika katika mauaji ya mmoja wa viongozi wa wanaotaka kujitenga katika jimbo la Punjab kwenye ardhi ya nchi hiyo, na kama ishara ya kupinga, imechukua hatua ya kumfukuza mwanadiplomasia wa India.

Ukandamizaji wa walio wachache

Kwa mtazamo wa waandamanaji wa Sikh, serikali ya "Modi" inafuata sera ya kuwakandamiza walio wachache kwa kuiga Wazayuni, na jambo hilo limesababisha kuwa pamoja Wahindu na Wazayuni wenye misimamo mikali. MD Kumar Singh, mtaalamu wa masuala ya kisiasa, anasema:

"Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya Kihindu ya India imeanzisha sera ya kuangamiza kizazi, haswa kwa Waislamu nchini India. Siasa za India katika kudhibiti Kashmir zinatokana na kuchochewa na siasa za jinai za Wazayuni dhidi ya watu wa Palestina. Kwa ajili hiyo, serikali ya India inadhani kwamba kwa kuunga mkono jinai za Wazayuni dhidi ya watu wa Gaza, uhusiano kati ya pande hizo mbili utapanuka zaidi.

Vyovyote iwavyo, uungaji mkono wa wananchi na wanafunzi wa India kwa wananchi wa Palestina hususan wa Gaza na kulaani jinai za Wazayuni kunaonyesha kwamba, wamesimama katika sehemu sahihi ya historia kwa kuwa na ufahamu sahihi. Wakati huo huo, kimya cha serikali ya India dhidi ya jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza si tu kwamba, hakitatui matatizo ya Wahindu wenye misimamo mikali, bali hilo litazidi kuchafua jina la India miongoni mwa Waislamu na wapenda uhuru wa dunia.

Wakati huo huo, kuondoka kwa Waziri Mkuu wa Hindu Narendra Modi kutoka mkondo wa sera za viongozi wakubwa wa kisiasa wa nchi hiyo kama vile akina Mahatma Gandhi katika kuunga mkono matakwa ya watu wa Palestina kunadhoofisha nafasi ya India kati ya nchi zinazopigania uhuru ulimwenguni. Hii ni kwa sababu viongozi wakubwa wa India, ikiwa ni pamoja na Jawaharlal Nehru, aliunga mkono kwa nguvu zote malengo ya Palestina na kuundwa Jumuiya ya Nchi Ziisizofungamana na Siasa za Upnde Wowote NAM, na kwa kufanya hivyo alijaribu kuikuza India na kuionyesha kuwa ni nchi huru, ambapo serikali ya Narendra Modi imo katika kubomoa na kuharibu yote hayo.

4175644

captcha