IQNA

Watetezi wa Palestina

Shehena ya Pili ya Msaada wa Kibinadamu wa Iran Kutumwa Gaza

14:26 - February 04, 2024
Habari ID: 3478302
IQNA - Meli ya pili iliyobeba misaada ya kibinadamu ya Iran kwa Ukanda wa Gaza imevuka Mlango-Bahari wa Hormuz, mkuu wa Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Iran alisema.

Pir Hossein Kolivand ameliambia Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) kwamba wananchi wa Iran wamewasilisha misaada mbali mbali kwa ajili ya watu wanaodhulumiwa wa Gaza.
Misaada hiyo ni pamoja na dawa na vifaa vya afya, chakula, nguo, na blanketi, alibainisha.
Kolivand ameongeza kuwa Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Iran iko tayari kukusanya vifaa zaidi kwani mahitaji ya kibinadamu ya watu wa Gaza ni makubwa zaidi kuliko yale yaliyotumwa katika eneo la Palestina hadi sasa.
Amebainisha kuwa shehena hii ya pili ya misaada ya kibinadamu ya Iran inayotumwa kwa njia ya bahari Ukanda wa Gaza na kuongeza kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amekuwa akifanya mazungumzo ya kimataifa kwa ajili ya uratibu wa kupeleka misaada zaidi katika ardhi ya Palestina inayozingirwa.
Hadi sasa zaidi ya tani 10,000 za misaada ya kibinadamu zimetumwa Gaza na watu wa Iran, aliendelea kusema.
Utawala haramu wa Israel ulianzisha hujuma mbaya kwenye Ukanda wa Gaza mnamo Oktoba 7 na kuua Wapalestina wasiopungua 27,238 na kujeruhi 66,452.
Mashambulizi ya Israel yamesababisha asilimia 85 ya wakazi wa Gaza kuwa wakimbizi wa ndani huku kukiwa na uhaba mkubwa wa chakula, maji safi na dawa, huku asilimia 60 ya miundombinu ya eneo hilo ikiharibiwa au kuharibiwa, kulingana na Umoja wa Mataifa.
 
4197791

captcha