IQNA

UN kufikisha misaada ya Iran nchini Yemen

10:36 - May 24, 2015
Habari ID: 3307026
Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula Duniani limeahidi kupeleka misaada ya Iran nchini Yemen. Meli ya Iran ilikuwa ipeleke misaada ya kibinadamu moja kwa nchini Yemen lakini ikashindwa kufanya hivyo kutokana na kuendelea hujuma za katika Bandari ya Hudaydah.

Meli hiyo iliyopewa jina la Nejat kwa maana ya uokoaji ni meli ya kwanza ya Iran ya misaada ya kibinadamu kuelekea huko Yemen na imelazimika kupitia Djibouti kama ilivyopendekezwa na Umoja wa Mataifa ili zoezi hilo la kuwafikishia misaada wananchi wa Yemen lifanyike chini ya umoja huo.
Meli hiyo imesheheni tani 2,500 kama vile vyakula kama vile, magharagwe,  ngano, mchele, maji, vifaa vya tiba na dawa.
Saudia iliwahi kuzuia ndege za misaada ya kibinadamu kutoka Iran kutua nchini Yemen.

Saudi Arabia imetekeleza hujuma nchini Yemen kuanzia Machi 26 ambapo baadhi ya duru zinasema zaidi ya watu 3,000 wakiwemo watoto, wanawake, wazee na raia wasio na hatia wameuawa. Aidha Saudia inayotumia silaha za Marekani imebomoa misikiti, mahospitali, nyumba za raia mbali na kuzuia misaada ya kibinaadamu isiwafikie raia wa Yemen.../mh

3306993

Kishikizo: meli iran misaada yemen
captcha