IQNA

Meli ya misaada ya Iran yaelekea Yemen

12:56 - May 12, 2015
Habari ID: 3292005
Meli ya misaada ya kibinadamu ya Iran kwa ajili ya wananchi wanaondelea kushambuliwa kinyama na Saudi Arabia huko Yemen inaendelea na safari yake baada ya kuondoka katika bandari ya Bandar Abbas, kusini mwa Iran.

Meli hiyo ya mizigo iliyopewa jina la Nejat yaani "wokovu" ina tani 2,500 za mahitaji ya lazima zaidi kikiwemo chakula, madawa na mahema.
Mbali na maafisa wa Hilal Nyekundu ya Iran, wanaharakati kadhaa wa kimataifa wamo ndani ya meli hiyo. Kati ya wanaharakati hao wako wafanyakazi wa kutoa misaada ya kibinaadamu, hudumza za afya na wanaharakati wa kutetea amani kutoka Marekani, Ufaransa na Ujerumani.
Waandishi wa habari na timu ya madaktari kutoka Iran ni miongoni mwa watu waliomo kwenye meli hiyo.
Meli hiyo itapitia Lango Bahari la Hormuz, Ghuba ya Oman, Bahari Arabu na yamkini ikatia nanga katika Ghuba ya Aden au kuelekea Bandari ya Hudaydah. Wakati huo huo Sayyid Amir Mohsen Zeyai, mkuu wa shirika la Hilal Nyekundu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelilaumu vikali shirika la kimataifa la Msalaba Mwekundu kwa kudharau masaibu yanayoendelea kuwatesa wananchi wasio na hatia wa Yemen.../mh

3290948

Kishikizo: iran meli misaada yemen
captcha