IQNA

Usomaji Qur'ani

Qari mmoja Misri apigwa marufuku miez sita kwa makosa ya qiraa

20:31 - January 07, 2024
Habari ID: 3478162
IQNA - Redio ya Qur'ani ya Misri imempiga qarii mmoja mkuu kutokana na kufanya makosa katika kusoma Qur'ani Tukufu hivi karibuni.

Sheikh Mohammed Hamed al-Kislawi haruhusiwi kusoma Qur’ani Tukufu katika Redio ya Qur'an na vituo vingine vya redio kwa muda wa miezi sita.

Haruhusiwi hata kurekodi kisomo chochote, kulingana na tovuti ya Al-Misri al-Yawm.

Wakati wa Swala ya Ijumaa wiki iliyopita, ambayo pia ilihudhuriwa na waziri wa wakfu wa nchi hiyo, al-Kislawi alifanya makosa alipokuwa akisoma aya za Surah Al-An'am.

Kosa hilo lilishutumiwa vikali na watumiaji wa mitandao ya kijamii na rais wa Jumuiya ya Wasomaji Qur'ani wa Misri pia aliapa kuchukua hatua dhidi ya qari hiyo.

Kwa mujibu wa Mohammed Nawar, mkuu wa Redio ya Quran, kamati iliundwa kuchunguza suala hilo.

Wanakamati hao kwa kauli moja walieleza kosa hilo kuwa halikubaliki, aliongeza.

Nawar amesema Redio ya Qur'ani na Jumuiya ya Wasomaji Qur'ani wamewataka maqari kufanya mazoezi na kujiandaa kikamilifu kabla ya kusoma Qur'ani katika matukio ya hadhara.

Pia alisema kosa kama lile lililofanywa na al-Kislawi haliwezi kuvumiliwa katika Redio ya Qur'ani ya Misri, ambayo ni redio ya kimataifa yenye mamilioni ya wasikilizaji kutoka duniani kote.

3486718

Habari zinazohusiana
Kishikizo: misri qari makosa
captcha