IQNA

Qiraa ya Qur'ani Tukufu

Qiraa ya Qur'ani ya Qari wa Azerbaijan yasifiwa kwenye Mitandao ya Kijamii (+Video)

22:01 - August 07, 2023
Habari ID: 3477394
BAKU (IQNA) – Klipu ya usomaji mzuri wa Qur'ani Tukufu wa kijana wa Jamhuri ya Azerbaijan Qari Muhammad Dabirov imependwa na mamilioni ya watazamaji kwenye mitandao ya kijamii.

Katika klipu hii anasoma Aya ya 77 ya Sura Al-Qasas: “Tafuteni manufaa ya maisha yajayo kupitia mali yenu bila ya kupuuza sehemu yenu ya maisha haya. Fanya wema kwa wengine kama vile Mungu alivyokutendea wewe. Msifanye maovu katika ardhi, kwani Mwenyezi Mungu hawapendi madhalimu.”
Klipu hii imepokea maoni milioni 8 hadi sasa, kulingana na tovuti ya habari ya Dunya al-Watan.
Qari huyo wa Jamhuri ya Azerbaijan kwa sasa anafanya kazi ya kurekodi usomaji wake wa Surah Al-Kahf katika kwa mujibu wa mbinu ya Hafs.
Ataisambaza kwenye mitandao ya kijamii baada ya kukamilika.

Habari zinazohusiana
captcha