IQNA

Diplomasia

Nasrallah: Jukumu la Shahidi Soleimani katika utulivu wa eneo hilo halisahauliki

19:35 - September 01, 2023
Habari ID: 3477532
TEHRAN (IQNA)- Katika kikao na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesisitiza nafasi ya Shahidi Jenerali Soleimani katika kuimarisha usalama wa eneo hili mbele ya Uzayuni na ugaidi.

Kwa mujibu wa IQNA,  Hossein Amir Abdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, ambaye alisafiri kwenda Beirut siku ya Alhamisi akitokea Syria, alikutana na Sayyid Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon ambapo wamejadilii matukio ya hivi karibuni ya kisiasa nchini Lebanon na kanda n

Katika mkutano huu, Amir Abdollahian alimfahamisha Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon kuhusu mazungumzo yake ya hivi karibuni na wakuu wa Saudi Arabia.

Ameyataja mazungumzo yake na viongozi wa Saudia kuwa chanya na kuongeza kuwa: 'Mchakato wa utekelezaji wa makubaliano kati ya nchi hizo mbili utakuwa ni kiashirio cha mtazamo wa nchi hizo mbili katika ukurasa mpya wa uhusiano kati ya Tehran na Riyadh."

Amir Abdollahian akiashiria pia mazungumzo yake na Rais wa Syria na maafisa wakuu wa nchi hii amesisitiza kuwa: "Katika hali ya kurejea uhusiano wa Syria katika hali ya kawaida na nchi za Kiarabu, harakati za kigeni katika kuamsha magaidi nchini Syria zinaashiria malengo ya maadui na utawala wa Kizayuni dhidi ya Syria na usalama wa eneo.

Katika mkutano huu, hali ya hivi punde zaidi ya Palestina na mizozo ya usalama na kijamii katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu yalijadiliwa.

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema katika kikao hicho: "Leo harakati za muqawama au mapambano Lebanon na Palestina ziko katika hali yenye nguvu zaidi, na iwapo Wazayuni watanzisha chokochooko, basi watapata majibu ya kujutia kutoka kwa wanamuqawama huo.

Akirejelea nafasi ya chanya ya Iran katika eneo na Lebanon, Sayyid Hassan Nasrallah amewaenzi na kuwakumbuka mashahidi wa muqawama  ambapo, ameitaja nafasi ya Shahidi Jenerali Qassem Soleimani katika kuleta utulivu wa usalama wa eneo hili na kukabiliana na Uzayuni na ugaidi kuwa ni jambo lisilosahaulika.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameonana pia na Spika wa Bunge la Lebanon mjini Beirut na pande mbili zimejadiliana masuala muhimu ya kieneo na kimataifa.

Hossein Amir-Abdollahian amesema, tathimini ya Iran kuhusu ustawi wa uhusiano kati yake na Saudi Arabia ni nzuri na jambo hilo lina manufaa si kwa Tehran na Riyadh tu, bali kwa eneo hili zima.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema pia katika mazungumzo yake hayo na Spika wa Bunge la Lebanon, Nabih Beri kwamba, kuna umuhimu mkubwa wa kudumishwa amani na utulivu katika eneo hili ikiwemo nchini Lebanon.

Amesema, kuchaguliwa mtu wa kushika nafasi ya urais wa Lebanon ni jambo la dharura na ni kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizi mbili za Lebanon na Iran.

Amir-Abdollahian amezungumzia pia matukio ya kusikitisha yaliyotokea hivi karibuni katika nchi za Ulaya za Sweden na Denmark ya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu na kusema kuwa, Bw. Mohammad Bagher Ghalibaf, Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) ametoa mapendekezo mazuri kwa mabunge ya nchi za Waislamu juu ya hatua za kuchukuliwa za kukabiliana na jinai kama hizo zilizofanywa hivi karibuni katika nchi za Sweden na Denmark.

Kwa upande wake, Bw. Nabih Beri Spika wa Bunge la Lebanon amesema, moja ya sababu kuu za kushinikishwa nchi yake ni kuweko huko muqawama wenye nguvu ambao unailinda vizuri Lebanon mbele ya vitisho vyote vya maadui. 

4166292

Habari zinazohusiana
captcha