IQNA

Siku ya Kimataifa ya Quds

Kiongozi wa Hizbullah atoa mwito wa kuweko mahudhurio makubwa katika Siku ya Kimataifa ya Quds

11:54 - April 08, 2023
Habari ID: 3476832
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon ameto mwito kwa wapenda haki kujitokeza kwa wingi katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds.

Akihutubia jana usiku, Sayyiid Hassan Nasrallah amesisitiza kuwa, haja kwa watu kujitokeza kwa hamasa na kwa wingi katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds na kutangaza himaya na uungaji mkono wao kwa wananchi wa Palestiina. 

Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, matukio ya Beitul-Muqaddas, Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Syria yana mafungamano na yapo katika mhimili wa jambo moja.

Imam Khomeini MA mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alitangaza Ijumaa ya mwisho ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Quds. 

Waislamu na wapenda haki wamekuwa wakifanya maandamano katika pembe mbalimbali za dunia kila mwaka katika Siku ya Kimataifa ya Quds, na kuonyesha hasira zao dhidi ya siasa za kibaguzi na kikatili zinazotekelezwa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.

Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka huu itafanyika Ijumaa ijayo ya tarehe 23 Ramadhani 1444 Hijria inayosadifiana na 14 Aprili 2023. Amesema Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka huu inasadifiana na usiku wa Laylatul Qadr na hivyo hii ni baraka maradufu kwa ulimwengu wa Kiislamu.

4132162

captcha