IQNA

Watetezi wa Qur'ani Tukufu

Kiongozi wa Hizbullah asema Waislamu wako tayari kuutetea Uislamu na Qur’ani Tukufu

21:31 - July 29, 2023
Habari ID: 3477352
BEIRUT (IQNA)- Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema jamii za Kiislamu haiwezi kustahamili kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu, akisisitiza kwamba Waislamu wako tayari kikamilifu kuchukua hatua za kuwajibika kuulinda Uislamu na kitabu chao kitakatifu.

Sayyid Hassan Nasrallah aliyasema hayo Jumamosi katika hotuba ya televisheni katika hafla iliyofanyika katika kitongoji cha Beirut kusini mwa Dahiyeh kwa mnasaba wa Siku ya Ashura ambayo hufanyika kumbukumbu kuuawa shahidi Imam Hussein (AS) - Imam wa tatu wa Waislamu wa Madhehebu ya Shia na mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW).

Sayyid Nasrallah alisifu ushiriki wa waombolezaji katika Siku ya Ashura na kusema huo ni "ujumbe wa wazi wa utii" kwa njia ya Mtume Mohammad (SAW) na Ahul Bayt wake watoharifu.

Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema: "Tunaahidi kwamba tutasalia kwenye njia ya Imam Hussein (AS) na kwamba tutabeba malengo yake na kukabiliana na madhalimu wote duniani."

Akiashiria matendo ya mara kwa mara ya kuivunjia heshima Qur’ani Tukufu barani Ulaya katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita, Sayyid Nasrallah alisema, “Uswidi na Denmark zinapaswa kujua kwamba taifa letu halivumilii kuvunjiwa heshima Qur’ani yetu Tukufu na matakatifu mengine ya Kiislamu.”

Amebaini kuwa sisitizo la kuvunjiwa heshima kitabu hicho kitakatifu cha Waislamu huko Denmark ni uchokozi dhidi ya Uislamu, kiongozi huyo wa Hizbullah alisema: "Tunasubiri msimamo thabiti wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) juu ya kuivunjia heshima Qur'ani, la sivyo, chombo hiki hakitakuwa tena na sifa za mtetezi wa  dini yetu.”

Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon amesema nchi za Kiislamu na mawaziri wao wa mambo ya nje lazima wachukue hatua juu ya uchokozi wa mara kwa mara dhidi ya Uislamu nchini Uswidi na Denmark, na kutuma ujumbe wa "maamuzi na wa kina" kwamba uchokozi mwingine utakabiliwa na vikwazo vya kidiplomasia na kiuchumi.

Nasrallah amesema: "Iwapo nchi hazitafanya hivyo, basi Waislamu shupavu na vijana wa Kiislamu duniani wako tayari kuchukua hatua za uwajibikaji za kuwaadhibu wale wanaoidharau na kuichoma moto Qur'an Tukufu."

Kiongozi wa Hizbullah amesema: "Vijana wote wa Kiislamu duniani watakuwa katika hali ya fedheha ikiwa serikali zao hazitasimamisha uchokozi huu, na ulimwengu utaona bidii ya vijana hawa ambao wako tayari kujitolea katika kuilinda Qur'ani Tukufu."

 

4158879

Habari zinazohusiana
captcha