IQNA

Jinai za Marekani

Kiongozi wa Hizbullah: Marekani ndio msingi wa laana na tauni

20:05 - November 12, 2022
Habari ID: 3476074
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Hizbullah Sayyid Hassan Nasrallah amejibu matamshi ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani dhidi ya Lebanon na Hizbullah na kusema: "Marekani ndio msingi wa laana na tauni, na Hizbullah ndiyo iliyoondoa shari na laana ya Marekani nchini Lebanon na kuangamiza tauni hiyo."

Sayyid Hassan Nasrallah aliyasema hayo usiku wa kuamkia leo katika maadhimisho ya Siku ya Shahidi yaliyofanyika mjini Beirut. Amesisitiza kuwa, Siku ya Shahidi ni siku ya mashahidi wote kuanzia Bahrain, Palestina, Iran na maeneo mengine ya dunia na kusema, adui Mzayuni amefikia hapa alipo kwa baraka ya damu za mashahidi wa kambi ya mapambano. 

Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amezungumzia machafuko ya hivi karibini nchini Iran na kufeli kwa njama za maadui na kusisitiza kuwa, Kwa mara nyingine tena Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imefanikiwa kuzima njama na fitina za Marekani na utawala haramu wa Israel.

Katika sehemu nyingine ya matamshi yake Sayyid Nasrallah amegusia suala la kuchaguliwa rais wa baadaye wa Lebanon na kusema: "Tunataka kujaza pengo katika taasisi hii haraka iwezekanavyo. Hatutaki rais wa kuilinda Hizbullah na muqawama, kwa sababu Hizbullah haihitaji kukingiwa kifua, lakini tunataka rais asiusaliti muqawama na mapambano."

Akizungumzia uchaguzi wa karibuni wa bunge la Israel, Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema kuwa, hakuna tofauti baina ya Benjamin Netanyahu na Wazayuni wengine, na wote ni watenda jinai na wahalifu. Amesema: "Kwa Hizbullah hakuna tofauti baina ya ushindi wa Netanyahu au Mzayuni mwingine, wote ni wahalifu, ijapokuwa kwamba ushindi wa Netanyahu utazidisha mgawanyiko ndani ya utawala wa Kizayuni wa Israel, na hapana shaka kwamba kushika madaraka watu wapumbavu huko Israel kutazidisha kasi ya kusambaratika utawala huo."

3481211

captcha