IQNA

Kadhia ya Palestina

Afisa wa Hizbullah asisitiza uungaji mkono wa Waislamu ulimwenguni kwa Palestina

12:55 - December 14, 2022
Habari ID: 3476247
TEHRAN (IQNA) Naibu Katibu MKuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sheikh Naim Qassem amesisitiza kwamba Palestina haiko peke yake kwa sababu ulimwengu wa Kiislamu unaiunga mkono.

Akihutubia katika hafla iliyofanyika mjini Beirut kwa mnasaba wa Siku ya Mshikamano na Taifa la Palestina, alisema mhimili wa muqawama (mapambano ya Kiislamu), mataifa ya Kiarabu na Kiislamu, na watu wenye heshima Palestina ni waungaji mkono wa ukombozi Palestina.

Sheikh Qassem ameitaja Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kama nembo ya muqawama kwani inaunga mkono kikamilifu taifa la Palestina na kadhia ya ukombozi wa Palestina.

Amesema, wakati baadhi wa madola ya Kiarabu yalielekea kwenye mapatano kwa utawala ghasibu wa Israel mwishoni mwa miaka ya 1970 na madola hayo yakashinikiza Wapalestina kuachana na muqawama dhidi ya wavamizi, Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalipata ushindi Februari 1979 na Iran ikawa muungaji mkono mkubwa wa Palestina. kuanzishwa kwa Jamhuri ya Kiislamu.

Kwingineko katika matamshi yake, afisa huyo wa Hizbullah amesema hakuna mtu anayepaswa kuzingatia muqawama huo kuwa ni sehemu ya muundo wa kisiasa wa nchi moja kwa sababu Waislamu wanakabiliwa na adui ambaye ameikalia kwa mabavu Palestina na pia idadi ya nchi nyingine za Kiarabu.

"Adui huyu aliingia Beirut na alilazimika kuondoka tu kutokana na muqawama," aliongeza.

Sheikh Qassem aliendelea kusema kuwa, utawala wa Kizayuni si adui wa Wapalestina pekee bali ni adui wa Waarabu, Waislamu na wanadamu wote kwa ujumla.

3481666

Kishikizo: hizbullah Naim Qassem
captcha