IQNA

Kiongozi wa Hizbullah

Kuangamia Israel si ndoto na matarajio tu bali ndio uhalisia utakashuhudiwa katika mustakabali

18:09 - March 11, 2023
Habari ID: 3476693
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema, eneo bila kuwepo Israel si ndoto na matarajio tu bali ndio uhalisia utakashuhudiwa katika mustakabali.
Kwa mujibu wa kanali ya Televisheni ya Al-Mayadeen, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon Seyyed Hassan Nasrallah amesema katika maadhimisho ya kumuenzi mmoja wa makamanda wa Muqawama, kwamba matukio yanayojiri kimataifa na katika eneo ni ushahidi kwamba kuzingirwa Yemen na Syria na nchi za ukanda huu kutafeli na kutagonga mwamba. Akaongeza kuwa, yanayotokea Palestina ni ya kihistoria na yenye umuhimu mkubwa sana na kwamba kielezo cha matukio ya eneo ni kwamba mhimili wa muqawama na mapambano una dhamira ya dhati, ikhlasi na uko tayari kujitolea mhanga, lengo lake likiwa ni kuikomboa Palestina.
Seyyed Hassan Nasrullah amesema, ndani ya utawala ghasibu wa Kizayuni wanazungumzia kuporomoka na kumalizika kwa ndoto ya Uzayuni, na huo ndio ukweli halisi. Kuna mwafaka wa rai ndani ya utawala wa Kizayuni kwamba mifarakano ya ndani na sababu za nje vitapelekea kutoweka utawala huo; na kile kilichoufanya utawala huo ufikie hapa ulipofika si kwa sababu ya hitilafu za ndani, bali ni msimamo thabiti wa eneo na muqawama ulioko Palestina na Lebanon pamoja na msimamo thabiti wa Syria na kupanuka kwa mhimili wa muqawama.

Katibu Mkuu wa Hizbullah ameeleza bayana kwamba, kuanzisha uhusiano na baadhi ya nchi hakutaupa kinga utawala haramu wa Kizayuni na wala hakutaweza kusimamisha operesheni za mashambulio dhidi ya Uzayuni; na akaongezea kwa kusema, leo mapambano katika Ukingo wa Magharibi na maeneo yanayokaliwa kwa mabavu yana umuhimu wa kiwango cha juu, yapo katika wakati muhimu sana katika mwenendo wa muqawama na hilo ndilo litakaoainisha hatima ya mustakabali.

Katika sehemyu nyingine ya hotuba yake, Seyyed Hassan Nasrullah amesema "Syria na Palestina ni sehemu ya eneo la Kiarabu, nasi tuna wajibu wa kimaadili, kitaifa na kidini kwa nchi hizi mbili jirani. Katika vita na adui na katika mhimili wa Muqawama Syria ilikuwa ikitoa mchango mkuu na licha ya vita vya kimataifa vilivyoanzishwa dhidi yake ingali inaendelea kutoa mchango huo.
Kuhusiana na kuanzishwa tena uhusiano kati ya Iran na Saudi Arabia, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema, "kurejeshwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Riyadh na Tehran ni jambo jema na tunalifurahia kwa sababu tuna hakika kwamba uhusiano huo una manufaa kwa mataifa ya eneo hili"

4127231

captcha