IQNA

Mawaidha

Uhusiano kati ya Taqwa na kujidhibiti kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu

22:56 - January 20, 2024
Habari ID: 3478224
IQNA – Taqwa (Kumcha Mungu) ni aina ya ulinzi maalum wa Nafs au Nafsi ambao pia huitwa kulinda eneo takatifu la Mwenyezi Mungu.

Ina maana kwamba Taqwa humkinga mtu kutokana na hasira na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, inahusiana na kujidhibiti.

Moja ya misingi ya kiimani katika  Uislamu ambayo inaweka nguzo ya utambuzi wa kujidhibiti ni kuamini utu na thamani ya mwanadamu kwa sababu kama mtu atatambua hadhi yake ya juu na heshima yake, atachukia mambo yasiyofaa na maovu. Kwa upande mwingine, mtu ambaye hajioni kuwa anastahiki na hadhi atakubali udhalilishaji wowote na wengine pia hawatakuwa salama kutokana na maovu yake.

Qur'ani Tukufu inauweka ubinadamu katika nafasi ya juu sana, jambo ambalo hatulioni katika itikadi au Imani zingine. Qur’ani Tukufu inawakumbusha wanadamu kwamba wameheshimiwa na Mwenyezi Mungu na anaweza kufikia hadhi ambayo hakuna malaika anayeweza. “ Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tulio waumba.” (Aya ya 70 ya Suratul Israa)

Heshima ya mwanadamu ni ya asili katika uumbaji wake. Ni kwa sababu ya uumbaji wake, akili, na uwezo wake pamoja na utawala wa kimungu na kuwa na viongozi wasiokosea.

Heshima ya mwanadamu pia inaweza kupatikana. Heshima maalum ya watu wenye Taqwa ni mfano. Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 13 ya Surah Al-Hujurat: “Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari."

Soma zaidi:

Kujidhibiti kwa Mtazamo wa Qur'ani

Kwa hiyo baada ya kigezo cha kwanza, ambacho ni uumbaji, ni Taqwa ndio kigezo cha ubora na utu wa wanadamu. Utu huu unaopatikana unaweza kuchukuliwa kuwa mojawapo ya matokeo muhimu zaidi ya kujidhibiti.

Taqwa, ambayo inatajwa mara kwa mara katika Qur’ani Tukufu kama thamani na ndiyo chimbuko la maadili mengine mengi, ni aina ya ulinzi maalum wa Nafsi. Kujidhibiti pia ni aina ya kujilinda mwenyewe.

3486869

captcha