IQNA

Namna Saumu ya Ramadhani inavyosaidia kukuza Taqwa (Ucha Mungu)

21:50 - April 18, 2023
Habari ID: 3476887
Tehran (IQNA) - Kufunga au Saumukatika Uislamu sio tu husaidia kuimarisha utendaji kazi wa sehemu tofauti za mwili lakini pia husafisha na kutakasa Batini (mwelekeo wa kiroho).

Saumu ni kati ya vitendo vya ibada ambavyo haviko tu katika  Uislamu bali pia vinafanywa na wafuasi wa imani zingine pia.

Kulingana na Qur’ani Tukufu, watu wote wanapaswa kufunga kama wajibu. Mwenyezi Mungu anasema katika aya ya 183 ya Surah al-Baqarah: " Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu.”

Kwa hivyo, kulingana na aya hii, kufanikisha taqwa ndio falsafa kuu ya kufunga.

Katika Uislamu, kufunga kunasaidia mwanadamu kwa matazamo wa kiroho na kimwili au kiafya na kwa msingi huyo  kufunga husaidia mwanadamu kujikurubisha zaidi na Mwenyez Mungu.

Uislamu unakamilisha dini zingine zote za Mwenyezi Mungu kwani una vipengee ambavyo havik katika dini zingine zilizotangulia.

Waislamu wanahitajika kufunga katika mwezi mtukufu wa Ramadhani na kujiepusha na vitendo kadha hasa kula, kunywa, kuvuta sigara, na kujamiiana wanandoa kutoka alfajiri hadi magharibi. Wakati kufunga katika Ramadhani ni wajib (lazima), ni Mustahab (imependekezwa) katika miezi mingine ya mwaka.

Ikiwa mtu anauliza jinsi kufunga kunaweza kumsaidia mtu kukuza Taqwa, inapaswa kusemwa kwamba kwa kufunga na kupitia shida zake, mtu anakaribia Mwenyezi Mungu. Ingawa ana njaa na kiu, anakataa kula na kunywa na hivyo uvumilivu wake husaidia kuongeza taqwa yake. Mtu ambaye anafunga, ana udhibiti wa matamanio yake na mwelekeo wake na hutii maagizo na maamurisho ya Mungu. Kwa hivyo atafikia Taqwa na ikiwa tayari ana Taqwa, itaimarishwa ndani yake.

Kulingana na Hadithi, mtu anayefunga hata akipumua au kulala huhesabiwa kuwa ni kitendo cha ibada, hata kupumua kwake na kulala. Hii inaonyesha umuhimu wa kufunga.

Jambo lingine juu ya kufunga ni kwamba wakati mtu anapitia njaa na kiu wakati wa kufunga licha ya kuwa na uwezo wa kula chakula na kunywa maji, itaimarisha roho ya kushukuru na shukrani kwa Mungu kwa baraka aliyompa.

Katika aya ya 184 ya Surah al-Baqarah, Mungu anasema: " (Mfunge) siku maalumu za kuhisabika. Na atakaye kuwa miongoni mwenu mgonjwa au yumo safarini basi atimize hisabu katika siku nyengine. Na wale wasio weza, watoe fidiya kwa kumlisha masikini. Na atakaye fanya wema kwa kujitolea, basi ni bora kwake. Na mkifunga ni bora kwenu, kama mnajua.  "

Fidiya hutoa fursa ya kupata thawabu kwa watu ambao hawawezi kufunga wakati wa Ramadhani. Fidiya ni kiasi fulani lakini ikiwa mtu anataka kutoa zaidi basi itakuwa ni bora kwake.

Ifahamike pia kwamba ni haramu kufunga saumu ya Ramadhani katika baadhi ya hali. Kwa mfano, Imam Sadiq (as) alisema mwanamke mjamzito au yule anayenyonyesha mtoto hairuhusiwi kufunga kwa sababu inaweza kumdhuru mtoto au kuidhuru mimba.

captcha