IQNA

Wanazuoni Mashuhuri wa Ulimwengu wa Kiislamu / 34

Kitabu cha msomi wa Kifaransa kuhusu sifa za hati za Misahafu ya kale

16:16 - November 21, 2023
Habari ID: 3477923
TEHRAN (IQNA) – Francois Deroche, mwanachuoni wa Kifaransa ambaye ni mtaalamu wa Codicology na Palaeography, amejadili sifa za Misahafu ya kwanza katika mojawapo ya vitabu vyake.

Jina la kitabu chake ni “Misahafu (Nakala za Qur'ani) za Bani Umayya: Muhtasari wa Kwanza”. Bila shaka ni moja ya kazi muhimu za kisasa zilizoandikwa juu ya mada ya maandishi ya Misahafu.

Tafsiri ya kitabu hiki katika lugha ya Kiarabu na Hisam Sabri pia imechapishwa huko Cairo.

Ni moja ya tafiti kuu zilizofanywa katika zama za kisasa kuhusu maandishi katika kurasa za Qur'ani Tukufu.

Katika kitabu hiki, Deroche anatoa historia ya mabadiliko ya nakala za maandishi ya zamani ya Qur'ani Tukufu.

Anasema hana imani na mbinu mpya za uandishi wa historia ya miswada na kwamba anajaribu kutumia mbinu mchanganyiko, ikiwa ni pamoja na uchambuzi wa hati, nakala na maandishi na historia ya sanaa ili kutambua maendeleo ya hati za Qur'ani kwa wakati.

Kitabu hiki kinachambua maandishi ya Qur'ani Tukufu ya zama za Bani Umayya, ambayo ni ya  karne ya kwanza ya Hijri.

Deroche alizaliwa Oktoba 24, 1952 huko Metz, Ufaransa. Yeye ni mtafiti na mtaalamu wa Codicology na Palaeography.

Ana digrii ya Egyptology (Utaalamu wa Historia ya Misri)  na amefanya kazi katika Bibliothèque nationale de France (maktaba ya kitaifa) huko Paris na vile vile Taasisi ya Mafunzo ya Anadolu ya Ufaransa.

Amekuwa profesa wa historia ya maandishi ya Qur'ani Tukufu katika Bibliothèque nationale de France tangu 2015.

Habari zinazohusiana
captcha