IQNA

Wanazuoni Mashuhuri wa Ulimwengu wa Kiislamu /22

Ignaty Krachkovsky; Mfasiri Maarufu zaidi wa Qur’ani Tukufu kwa Kirusi

22:02 - May 22, 2023
Habari ID: 3477031
TEHRAN (IQNA) – Ignaty Krachkovsky alikuwa Mrusi mtafiti wa masuala ya mashariki na ya lugha Kiarabu ambaye anajulikana kwa tarjuma ya Qur’ani Tukufu katika lugha ya Kirusi.

Krachkovsky (Machi 1883, Vilnius - 24 Januari 1951, Leningrad) alikuwa Mrusi na Msovieti mtaalamu wa masuala ya Kiarabu na alikuwa msomi wa Chuo cha Sayansi cha Urusi kuanzia 1921; na 1925 Chuo cha Sayansi cha Shirikisho la Sovieti na mmoja wa waanzilishi wa shule ya Sovieti ya Masomo ya Kiarabu.

Kitabu chake cha Maandishi ya Kiarabu kilitunukiwa Tuzo la Stalin (mwaka wa 1951).

Pia alikuwa miongoni mwa wanazuoni waliochangia katika nakala ya awali kabisa ya  Ensaiklopidia ya Kiislamu. Aliandika makala ya ensaiklopidia kuhusu Abi Bakr Muhammad ibn Yahya al-Suli.

Krachkovsky aliandika tarjuma maarufu zaidi ya Qur’ani Tukufu kwa lugha ya Kirusi.

Kati ya tarjuma ya Qur’ani Tukufu kwa Kirusi ilianza mwanzoni mwa miaka ya 1700 kwa amri ya Peter Mkuu, Tsar wa Urusi yote kutoka 1682, na Mfalme wa kwanza wa Urusi yote kutoka 1721 hadi kifo chake mnamo 1725.

Hivi sasa, kuna tarjuma 15 za Kirusi za Qur’ani Tukufu. Mnamo 1716, Pyotr Postinkov alichapisha tarjuma ya kwanza ya Our’ani katika lugha ya Kirusi ambayo iliteggemea tarjuma ya ya Kifaransa ya  Qur’ani Tukufu André du Ryer. Gordiy Sablukov alichapisha tarjuma ya  kwanza ya Kirusi ya Qur’ani kutoka Kiarabu mnamo 1873.

Watarjumi wengine wa Qur’ani Tukufu kwa Kirusi ni pamoja na: Mikhail Veryovkin (1790), Alexey Kolmakov (1792), K. Nikolaev (1864), Gordiyya Sablukov (1877), Valeria Iman Porokhova (1993), Fazil Qarauqlu (1994), Raul Bukarayev. (2006) na U. Z. Sharipov na R.M. Sharipova (2006).

Pia Shamil Alaeddinov ameandika tafsiri ya maana za Qur’ani Tukufu  katika juzuu nne.

Tarjuma ya Krachkovsky inaonekana na wengi kuwa yenye thamani. Tarjuma ya Qur'ani kwa Kirusi kabla yake ilikuwa na dosari kuu mbili. Kwanza, nyingi kati ya hizo zilikuwa zimetartjumiwa kutoka lugha nyingine isiyokuwa Kiarabu. Na pili, walikuwa wa mila ya mashariki ya Tsarist Russia ambapo aina ya uadui na Waislamu na Uislamu inaweza kugunduliwa.

Krachkovsky aliondoka hapo. Alikuwa amekaa kwa miaka mingi katika nchi za Kiarabu na kujifunza lugha ya Kiarabu hivyo alikuwa anafahamu lugha ya Kiarabu kwa undani kabisa. Pia alifahamu fasihi ya Kiarabu, ambayo ilimsaidia kutambua mtindo wa kipekee na maalum wa Qur’ani Tukufu.

Alifanya juhudi zote kuwasilisha mtindo huu katika tafsiri au tarjuma yake. Pia alijaribu kuandika tarjuma kwa namna ambayo ingewezekana kusoma kwa wasomaji katika viwango tofauti.

Krachkovsky alitumia miaka 40 katika kutafsiri Qur’ani Tukufu kwa Kirusi lakini ilichapishwa mnamo 1963, miaka 12 baada ya kifo chake. Ni mojawapo ya tarjuma bora zaidi za Kirusi za Qur’ani Tukufu na bila shaka ni mojawapo ya tafsiri bora zaidi za Kitabu Kitakatifu katika lugha yoyote ile.

captcha