IQNA

Jinai za Israel

Israel yadondosha mabomu misikitini, makanisani na shuleni Gaza

19:20 - October 30, 2023
Habari ID: 3477815
AL-QUDS (IQNA) - Idadi ya misikiti iliyoharibiwa katika mashambulizi ya anga ya utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza inakaribia 50.

Ofisi ya vyombo vya habari nchini ilisema Jumapili kwamba mashambulizi ya mara kwa mara ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza tangu Oktoba 7 yamesababisha uharibifu wa misikiti 47 na makanisa matatu.

"Uvamizi wa Israel kwenye Ukanda wa Gaza umesababisha uharibifu wa misikiti 47 na kuharibu makanisa matatu na shule 203 pamoja na majengo 80 ya serikali," mkurugenzi wa ofisi hiyo, Salama Maarouf, alisema katika mkutano na waandishi wa habari.

Alisema idadi ya wahudumu wa afya waliouawa imefikia 116 pamoja na waokoaji 18 na vikosi vya ulinzi wa raia na waandishi wa habari 35.

Wizara ya Afya katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa, hadi kufikia jioni ya leo idadi ya Mashahidi wa mashambulizi ya kinyama ya utawala wa Kizayuni katika eneo hilo imeongezeka na kufikia watu 8,306.

Msemaji wa Wizara ya Afya iliyo chini ya serikali ya Hamas huko Gaza amesema, katika siku ya 24 ya vita hivyo, idadi ya Mashahidi imeongezeka na kufikia 8,306.

Siku ya Jumamosi, tarehe 7 Oktoba 2023, wanamapambano wa Muqawama wa Palestina walianzisha operesheni ya kushtukiza iliyopewa jina la Kimbunga cha Al-Aqsa kutokea Gaza (kusini mwa Palestina) dhidi ya ngome za utawala wa Kizayuni unaoikalia Quds kwa mabavu. Katika hatua ya kulipiza kisasi na kufidia kipigo kikali na pigo kubwa ulilopata, utawala wa Kizayuni umechukua hatua ya kufunga vivuko vyote vya Gaza na hivi sasa unaendeleza mashambulio ya mtawalia dhidi ya maeneo ya makazi ya watu na vituo vya tiba vya Ukanda huo.

3485801

Habari zinazohusiana
Kishikizo: gaza jinai za israel
captcha