IQNA

Kadhia ya Palestina

Ayatullah Khamenei: Kushindwa Israel katika shambulio la "Kimbunga cha Al-Aqsa" ni pigo lisiloweza kusawazishika

22:21 - October 10, 2023
Habari ID: 3477707
TEHRAN (IQNA)-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema utawala wa Kizayuni wa Israel utachapwa "kibao kikali zaidi" kwa mauaji inayoendelea kufanya dhidi ya wananchi wa Palestina katika Ukanda wa Gaza iliouwekea mzingiro.

"Wazayuni wanapaswa wajue kwamba watachapwa kibao kikali zaidi kwa mauaji ya watu wa Gaza", ameeleza Ayatullah Khamenei mapema leo katika mahafali ya pamoja ya makadeti wahitimu wa mafunzo ya vikosi vya ulinzi kwenye Chuo Kikuu cha Maafisa wa Jeshi cha Imam Ali (AS) kilichoko mjini Tehran.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi amesisitiza kuwa, kushindwa utawala wa Kizayuni katika shambulio la "Kimbunga cha Al-Aqsa" ni pigo lisiloweza kusawazishika kwa upande wa kijeshi na kiintelijensia; na ni zilzala angamizi ambayo ni baidi kwa utawala huo ghasibu kuweza kurekebisha hali ya utawala wake kutokana na mapigo makali ya tukio hilo uliyopata licha ya misaada unayopewa na Wamagharibi.

Ayatullah Khamenei amebainisha kuwa sababu ya kutokea kimbunga hicho angamizi ni dhulma, jinai na unyama wa mtawalia unaofanywa na utawala bandia wa Kizayuni dhidi ya haki za watu wa Palestina; na utawala huo hauwezi kuficha sura yake ya unduli na khulka yake ya uhayawani kwa kusema uwongo na kujifanya mdhulumiwa kutokana na unavyoishambulia Gaza na kuwaua watu wake kwa halaiki na wakati huohuo kutoa kauli za porojo za kuwabebesha wasio Wapalestina dhima ya kazi ya kishujaa iliyofanywa na vijana wa Kipalestina na mkakati wa kimahiri walioutekeleza.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, baada ya Jumamosi ya Oktoba 7, ya siku ya hamasa ya kishujaa ya vijana wa Palestina, utawala wa Kizayuni si utawala tena uliokuwa kabla na akaongezea kwa kusema: "sababu ya balaa hili kubwa ni hatua za Wazayuni wenyewe; kwa sababu mnapopindukia kikomo cha unyama na uhayawani, lazima mtarajie kufikwa na "kimbunga".

Ayatullah Khamenei ameashiria uovu na ukhabitihi wa utawala ghasibu wa Israel na akasema: hakuna taifa lolote la Kiislamu katika historia ya zama hizi ambalo limekabiliwa na uadui na ukatili mkubwa kama wa utawala wa Kizayuni, na hakuna taifa lolote ambalo limekabiliwa na mashinikizo, mzingiro na uhaba mkubwa kama taifa la Palestina; na akaongezea pia kwa kusema: Marekani na Uingereza hazijawahi kuunga mkono serikali yoyote katili na ya kidhalimu kama zinavyouunga mkono utawala bandia wa Israel.

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameyataja mauaji ya Wapalestina wanaume na wanawake pamoja na watoto na vikongwe, kuuvunjia heshima Msikiti wa Al-Aqsa, kuwakanyaga na kuwapiga mateke waumini wanaosali wa Palestina na kuwatomeza walowezi wa Kizayuni wenye silaha wawashambulie Wapalestina kuwa ni miongoni mwa jinai za utawala wa Kizayuni na akaongezea kwa kuhoji: Je! taifa lenye ghera la Palestina na lenye historia ya maelfu ya miaka lilikuwa na chaguo jengine la kutumia kukabiliana na dhulma na jinai zote hizi zaidi ya kuibua "kimbunga"?.

/3485518

Habari zinazohusiana
captcha