IQNA

Hamas yailaani vikali Bahrain kwa kumtuma balozi Israel

15:38 - September 02, 2021
Habari ID: 3474250
TEHRAN (IQNA) - Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, imesema ufalme wa Bahrain kweli umeonyesha kuhusika kwake katika jinai zinazofanywa na utawala wa haramu wa Israeli dhidi ya Wapalestina kwa kumteua balozi wake wa kwanza kuhudumu katika utawala wa Israel.

"Uteuzi wa balozi wa utawala wa Bahrain katika utawala wa Kizayuni unaonyesha kusisitiza kwake juu ya dhambi ya kitaifa ambayo ilitenda wakati ilisaini makubaliano ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala huo ghasibu," msemaji wa Hamas Hazem Qassem alisema Jumatano.

Qassem alibainisha kuwa hatua hiyo inawakilisha "uungaji mkono wazi" wa Bahrain kwa sera za Israeli dhidi ya Wapalestina na "ushirika wake kamili" katika zinazotendwa na Tel Aviv.".

Khaled Yousif al-Jalahmah, ambaye aliteuliwa kuwa balozi wa kwanza wa ufalme wa Bahrain katika utawala wa Kizayuni mnamo Machi, aliwasili katika utawala huo Jumanne.

Wakati huo huo, Sheikh Hussain al-Daihi, naibu katibu mkuu wa Jumuiya ya Kitaifa ya Kiislamu ya  Al Wefaq ya Bahrain, na ambayo imepigwa marufuku nchini humo, amesema huyo mpya anawakilisha tu utawala na ufalme wa Bahrain na sio wananchi waliowengi.

"Tunamwambia al-Jalahmah, unajiwakilisha mwenyewe na yule aliyekutuma wewe tu, na hauwakilishi Bahrain," Sheikh AL-Daihi ameandika katika Twitter.

"Taifa la Bahrain litabaki upande wa Wapalestina na kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel ni usaliti na aibu."

Mwaka 2020, Bahrain na Umoja wa Falme za Kiarabu pamoja na Morocco na Sudan ziliafiki  kuanzisha uhusiano na utawala haramu wa Israel kufuatia mashinikizo ya Marekani. Kitendo hicho kiliibua ghadhabu kote Palestina na kwingineko kote ulimwenguni wa Kiislamu ambapo hatua hiyo imetajwa kuwa ni usaliti mkubwa wa serikali za Kiarabu kwa malengo matukufu ya ukombozi wa Palestina.

3475607

captcha