IQNA

Maandamano ya Wabahrain kulaani mauaji ya kijana mwanamapinduzi

23:25 - September 09, 2021
Habari ID: 3474277
TEHRAN (IQNA)- Wananchi wa Bahrain wameandamana kulaani kuuawa shahidi Mohammad Nas, kijana mwanadampinduzi aliyekuwa mfungwa wa kisiasa katika jela za kuogofya za utawala wa kiimla wa Aal Khalifa.

Kwa mujibu wa taarifa kijana huyo amepoteza maisha kutokana na uzembe wa makusudi wa maafisa wa gereza ambao walikataa kumpa matibabu.

Katika kulalamikia hali hiyo, wananchi wa Bahrain Jumanne usiku waliandamana kulaani sera za utawala wa Aal Khalifa za kuwakamata na kuwafunga wanaharakati wanaotetea uhuru wa kisiasa.

Chama kikuu cha upinzani Bahrain cha Al Wifaq al Islami, ambacho kimepigwa marufuku, pia kimetoa taarifa kulaani kuuawa shahidi Muhammad Nas na kusema kijana huyo amepoteza maisha kutokana na uzemba wa makusudi na kwamba alikuwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kwa muda wa miezi mitano baada ya kuambukizwa corona akiwa gerezani. Taarifa hiyo imesema kijana huyo mwanadampinduzi alikuwa anaugua ugonjwa wa Anemia lakini pamoja na hayo wakuu wa gereza hawakumpa matibabu yanayofaa.

Mwamako wa watu wa Bahrain dhidi ya utawala wa kifalme ulianza Februari 14 2011. Mwamko huu ni tofauti na harakati zingine za mwamko katika uliwengu wa Kiarabu ukiwemo mwamko uliopelekea kuangushwa Zine El Abidine Ben Ali wa Tunisia au Husni Mubarak wa Misri. Tofauti ya mwamko wa watu wa Bahrain ni kuwa, nchi hiyo inapakana na Saudi Arabia ambayo ni mpinzani na adui mkubwa zaidi wa mwamko na mapinduzi ya wananchi katika nchi za Kiarabu.

Kwa msingi huo, mwezi mmoja baada ya kuanza mwamko wa Februari 14, utawala wa Saudia ulituma wanajeshi wake Bahrain kwa lengo la kuwakandamiza raia wa nchi hiyo. Askari hao vamizi wa Saudia waliingia Bahrain katika fremu ya 'Ngao ya Kisiwa' ya Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi. 'Ngao ya Kisiwa' ni mapatano ya ushirikiano wa kijeshi wa nchi za Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi kwa lengo la kukabiliana na hujuma ya kigeni.

Hivi sasa ukiwa ni mwaka wa 10 tokea uanze mwamko wa watu wa Bahrain, wanajeshi wa Saudia na pia wale wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) bado wako nchini Bahrain na wanashirikiana na askari waliokodiwa wa utawala wa ukoo wa Aal Khalifa katika kuwakandamiza wananchi ambao wamekuwa wakiandamana kupigania mageuzi hasa ya kutaka kuwepo utawala unaochaguliwa moja kwa moja na wananchi.

 

 

 

/3996117

captcha