IQNA

Laylatul Qadr

Laylatul Qadr huko Makka: Waislamu Milioni 2.5 wajumuika Katika Msikiti Mkuu

22:06 - April 06, 2024
Habari ID: 3478638
IQNA-Katika mkusanyiko wa kihistoria, Waislamu milioni 2.5 walikusanyika na kusali katika Msikiti Mkuu wa Makka, Masjid al Haram, Saudi Arabia, siku ya Ijumaa kuhusiha mojawapo ya usiku mtukufu zaidi wa Ramadhani mwaka huu.

Mamlaka ya Masuala ya Misikiti Miwili Mitukufu ya Makka na Madina iliripoti kwamba mipango sahihi ilihakikisha mtiririko usio na dosari wa idadi kubwa ya Mahujaji wa Umrah wakati wa sala za usiku zilizoswaliwa Ijumaa ya mwisho ya Ramadhani.

Kwa waumini, usiku huu una umuhimu mkubwa kwani unaashiria Laylat Al Qadr (Usiku wa Hatima)—kilele cha umaanawi katika mwezi mtukufu wa Ramadhani wakati Quran ilipoteremshwa kwa Mtume Muhammad (SAW).

Ili kuhakikisha usalama na utulivu wa tukio mjumuiko huo mkubwa wa waumini, vikosi vya ulinzi viliongezwa maradufu katika eneo hilo takatifu, na kuwezesha usimamizi wa umati wa watu waliokusanyika kuswali usiku huu mtukufu wa Ramadhani.

Vyombo vya habari vya ndani viliripoti kwamba idadi ya walishiriki katika sala za Tarawih na Tahjjud mwaka huu siku ya Ijumaa ilikuwa ni mpya kwa Msikiti Mkuu. Viwanja vyake vilifikia uwezo kamili, vikiwachukua mahujaji wa Umra na waabudu waliokusanyika kuswali Isha, Tarawehe, na Qiyam Al Layl.

Ingawa siku mahususi ya Usiku wa Qadr bado haifahaimiki, Mtume Muhammad (SAW)  amenukuliwa akisema iko mikesha 10 ya mwisho ya Ramadhani, huku wanazuoni wengi wakisema uwezekano mkubwa ni kuwa siku hiyo inaweza kuwa mkesha wa 19, 21, 23 au 27 katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

3487825

 

Kishikizo: makka umrah ramadhani
captcha