IQNA

Roboti zinatumika katika Msikiti wa Makka kujibu maswali kwa lugha 11

12:30 - May 16, 2022
Habari ID: 3475258
TEHRAN (IQNA)- Hivi sasa roboti zinatumika kuwaongoza Waislamu wanaofika katika Msikiti Mtakatifu wa Makka kwa ajili ya kutekeleza ibada ya Hija Ndogo ya Umrah.

Kwa mujibu wa taarifa roboti hizo zinajibu maswlai na kuwapa fursa watumizi kuwasiliana na wasomi wa Kiislamu walioko mbali.

Roboti hizo kwa sasa zinazungumza lugha 11 ambazo ni Kiarabu, Kiingereza, Kifaransa, Kirusi, Kifarsi, Kituruki, Kimalay, Kiurdu, Kichina, Kibengali na Kihausa.

Pia roboti hizo zenye magurudumu manne zina skirini za inchi 12 na zinaweza kusimama na kutembea kwa kutegemea eneo la kazi.

Aidha zina kamera za kiwango cha juu na hivyo taswira zinazotumwa ni safi kabisa mbali na kuwa zina hedfoni na mikrofini za kiwango cha juu.

Mfumo wa roboti hizi unatumia mtandao wa Wi-Fi wenye kasi ya GHz 5 na hivyo kuuwezesha kutuma na kupokea taarifa haraka.

3478919

Kishikizo: makka umrah roboti
captcha