IQNA

Utalii

Watalii Waislamu wanaotembelea Russia waliongezeka kwa 15% mnamo 2023

19:12 - January 24, 2024
Habari ID: 3478244
IQNA - Idadi ya watalii Waislamu wanaozuru Russia iliongezeka mwaka 2023 kwa asilimia 15 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia. Hii ni kulingana na Huduma ya Takwimu nchini humo.

Waislamu kutoka sehemu mbalimbali za dunia husafiri hadi Russia kutembelea maeneo ya kihistoria ya nchi hiyo, hasa katika Jamhuri ya Tatarstan ambako kuna majengo mengi ya Kiislamu yenye usanifu wa Kiislamu pamoja na miundombinu mizuri ya utalii yenye kufuata msingi Halal, yaani huduma kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu.
Katika miaka ya hivi karibuni, huduma za utalii za Halal zimeendelea nchini Russia. Kiwango cha serikali cha kutoa bidhaa na huduma Halal kiliidhinishwa mwaka jana.
Idadi ya watalii kutoka Uturuki, Iran na Tajikistan waliozuru Russia mwaka 2023 iliongezeka maradufu ikilinganishwa na 2022 huku idadi ya wale kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu ikiongezeka mara tano.
Mji wa Bolgar ulio kwenye ukingo wa kushoto wa Mto Volga ni kivutio kikubwa cha watalii huko Tatarstan.
Mji huo ulio karibu na Kazan, mji mkuu wa jamhuri hiyo, una maeneo mengi ya Waislamu ambao wamekuwa huko kwa karne kadhaa.
Volga Bulgaria lilikuwa jimbo la kihistoria la Kibulgaria lililokuwepo kati ya karne ya 7 na 13 Miladia karibu na makutano ya Mto Volga na Kama, eneo ambalo leo ni Russia ya Ulaya.
Mnamo mwaka wa 922 Miladia, mfalme wa Volga Bulgaira alikubali Uislamu na watu wa eneo hilo walimfuata na kusilimu.
Kila mwaka, kumbukumbu ya kuwasili kwa Uislamu katika eneo hilo huadhimishwa katika mwezi wa Mei.
Kuna jumba la makumbusho la turathi za Kiislamu katika Jamhuri ya Tatarstan ambalo linashikilia nakala kubwa zaidi duniani iliyochapishwa ya Kurani Tukufu.
Nakala hupima mita 2 kwa 1.5 na ina uzani wa karibu kilo 800.
Russia  ina idadi kubwa ya Waislamu. Inakadiriwa kuwa zaidi ya Waislamu milioni 20 nchini humo, wengi wao wanaishi Tatarstan.

3486932

captcha