IQNA

Umrah

Zaidi ya Waislamu Milioni 13.5 walishiriki Umrah mwaka 2023

21:21 - January 09, 2024
Habari ID: 3478173
IQNA - Idadi ya Waislamu walioshiriki katika Hija ndogo ya Umrah mwaka 2023 ilifikia zaidi ya milioni 13.5, rekodi ya juu kwa wageni wa kimataifa walioshiriki ibada ya Umrah, waziri wa Hija na Umrah wa Saudia alisema Jumanne.

Tawfiq al-Rabiah alisema idadi hiyo iliongezeka kwa asilimia 58 kutoka mwaka uliopita, wakati takriban watu milioni 8.5 walifanya ibada hiyo, Al-Arabiya iliripoti Jumanne.

Umra ni safari ya kwenda Makka, Saudi Arabia, ambayo inaweza kufanywa wakati wowote wa mwaka, tofauti na Hija, ambayo ina tarehe maalum na ni moja ya nguzo tano za Uislamu.

Al-Rabiah alisema ongezeko hilo la wanaoshiriki ibada ya Umrah limetokana na vifaa na huduma zinazotolewa na serikali ya Saudia, ambayo imewekeza zaidi ya dola bilioni 1.3 katika kuendeleza miundombinu ya maeneo matakatifu.

Aliyasema hayo katika Kongamano na Maonyesho ya Huduma za Hijja na Umra, lililoanza Januari 8 hadi 11 katika Ukumbi wa Jeddah Superdome.

Kongamano hilo lililoandaliwa na Wizara ya Hija na Umra kwa ushirikiano na Programu ya Huduma ya Wageni wa Mwenyezi Mungu, sehemu ya Dira ya Saudia 2030, lilikuwa na vipindi na warsha kuhusu maendeleo ya baadaye ya miji na maeneo matakatifu na mada nyingine zinazohusiana.

Katika mkutano huo, naibu waziri wa mambo ya nje, Waleed el-Khereiji, alitangaza uzinduzi wa visa vya kielektroniki, au e-visa, Desemba 2023 kwa wanaoshiriki Hija ndogo ya Umrah, ambayo itawawezesha kupata vibali bila kulazimika kufika ubalozi. .

Alisema visa hivyo vya kielektroniki pia vitasaidia kukabiliana na changamoto za kiafya na kiusalama, kama vile visa ghushi, ambazo wizara imekuwa ikifanya kazi ya kuzizuia kwa uratibu na mamlaka za usalama.

3486746

Habari zinazohusiana
Kishikizo: umrah 1445 saudia
captcha