IQNA

Saudia yatangaza watu 70,000 wanaweza kutekeleza ibada ya Umrah kwa siku moja

13:33 - September 08, 2021
Habari ID: 3474272
TEHRAN (IQNA) – Wizara ya Hija na Umrah Saudi Arabia imeongeza idadi ya waumini wanaoweza kutekeleza ibada Umrah kila siku hadi 70,000.

Waumini wanaweza kujisajili kushiriki katika Hija ndogo ya Umrah na kupata kibali  chao.

Kuna aplikesheni ijulikanayo kama  Eatmarna ambayo inatumika kuwasajili wanaotaka kutekeleza ibada ya umrah.

Chini ya mwezi mmoja uliopita, kundi la kwanza la wafanyaziara ya Umrah kutoka nje ya nchi walifika Saudi Arabia ambao kundi hilo lilikuwa ni la  Wanigeria ambao ni raia wa kwanza wa kigeni kutua katika eneo lililoonekana kuwa takatifu zaidi kwa Waislamu.

 

Wizara ya Hajj na Umrah ya Ufalme ilithibitisha mahujaji wa Hija Ndogo ya Umrah kutoka Nigeria walifika saa 9.00 alasiri mnamo Agosti 13, katika Uwanja wa ndege wa Mfalme Abdulaziz wa Jeddah. Wakawa mahujaji wa kwanza wa mwaka.

 

Zitakuwa kampuni za makazi kupokea mahujaji wa Umrah kutoka uwanja wa ndege na hoteli na kusimamia kuingia kwao kwenye Msikiti Mkuu. "Wako tayari," mjumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Hija na Umrah Hani Ali Al-Amiri alisema.

Wizara ya Hija na Umrah Saudia imesema inafanya kazi kwa uratibu na mamlaka zingine ili kuandaa  mazingira salama kwa wanaotekeleza ibada ya Hija ndogo ya Umrah.

Kwa wenyeji na wakaazi, chanjo ya COVID-19 ni sharti la kutekeleza Umrah na kutembelea na kusali katika misikiti miwili mitakatifu ya Makaa na Madin. Wanaotoka nje ya ufalme wa Saudia ni lazima wawasilishe cheti rasmi cha chanjo kutoka nchi zao, pamoja na chanjo hiyo kutoka kwa orodha ya chanjo zilizoidhinishwa na Saudi Arabia. Wanaowasili Saudia pia wanapaswa kuzingatia taratibu za karantini.

Naibu waziri alisema kuwa idadi ya abiria kwenye chombo cha kusafirishia haitazidi asilimia 50 ya uwezo wake, huku wasafiri wakitakiwa kutokaribiana.

3475659

Kishikizo: umrah saudia
captcha