IQNA

Harakati za Qur'ani Tukuuf

Serikali ya Maldivi yatangaza azma ya kustawisha mafundisho ya Qur'ani Tukufu

9:14 - December 21, 2023
Habari ID: 3478067
IQNA - Rais wa Maldivi (Maldives) Mohamed Muizzu amesisitiza azma ya serikali yake ya kuendeleza ufundishaji wa Qur'ani Tukufu na kuunga mkono walimu wa Qur'ani nchini humo.

Katika hafla ya hivi majuzi, Muizzu alisisitiza umuhimu wa kina wa Qur'ani Tukufu katika elimu ya dini na katika kuongoza maisha ya kila siku.

Akishukuru kujitolea kwa walimu wa Qur'ani Tukufu, alipongeza juhudi zao na baraka nyingi zinazopatikana kutokana na kufundisha na kujifunza kitabu hicho kitakatifu.

Amesisitiza kuwa ufundishaji na kujifunza Qur'ani Tukufu yote ni ibada. Alitoa shukrani kwa walimu wa Qur'ani kwa kujitolea kwao kutoa elimu ya dini, akibainisha jukumu muhimu la Qur'ani Tukufu katika kuwaongoza watu binafsi katika maisha yao ya kila siku, na ushawishi wake mkubwa katika utamaduni na mila za watu wa Maldivi.

Muizzu aliangazia nafasi muhimu ya Qur'ani Tukufu katika tamaduni na mila za Wamaldivi.  Amesema Qur'ani Tukufu, kwa mujibu wake, ni mwongozo unaotengeneza maisha ya kila siku ya watu, na msingi wa mila na maadili yao.

Vile vile alisisitiza utakatifu wa kufundisha na kujifunza Qur'ani Tukufu, akibainisha baraka kubwa zinazoambatana na ibada hizo.

Rais pia alizungumzia dhamira ya serikali katika kukuza elimu ya Kiislamu. Ameeleza kuwa serikali imejitolea kuendeleza ufundishaji wa Qur'ani Tukufu na akasisitiza juhudi zake za kuwaunga mkono walimu wa Qur'ani Tukufu .

Alihitimisha hotuba yake kwa kusisitiza dhamira ya serikali yake ya kudumisha na kuendeleza elimu ya Kiislamu na ufundishaji wa Qur'ani Tukufu.

Maldives au Maldivi ni nchi huru kwenye funguvisiwa la Maldivi katika Bahari Hindi katika eneo la kusini mwa Asia. Nchi hiyo inajumuisha  visiwa 1,192 na kati ya hivyo takriban 200 hukaliwa na watu. Idadi ya watu katika nchi hiyo ndogo inakadiriwa kuwa nusu milioni na asilimia 100 ya raia wa nchi hiyo ni Waislamu.

348650

captcha