IQNA

Wanamichezo Waislamu

Bingwa wa mieleka atunuku medali zake za Dhahabu kwa Jumba la Makumbusho la Haram ya Imam Ridha (AS)

15:45 - November 05, 2023
Habari ID: 3477845
TEHRAN (IQNA) - Mwanamieleka bingwa wa dunia wa Iran, Amirhossein Zare, ameweka wakfu nishani zake mbili za dhahabu alizoshinda hivi karibuni katika mashindano ya bara na dunia kwa Jumba la Makumbusho la Haram ya Imam Ridha (AS) ilyoko Mashhad, kaskazini mashariki mwa Iran.

Zare alitoa ofa hiyo katika hafla ya Alhamisi huko Mashhad ambayo ilihudhuriwa na maafisa kadhaa wa kitaifa na wa mkoa wa michezo na kitamaduni katika Kituo cha Maonyesho na Mikutano cha Imam Ridha (AS).

Akisema kwamba ametoa nishani zake zote kwa m kwa Jumba la Makumbusho la Haram ya Imam Ridha (AS)  tangu mwanzo wa shughuli zake za kitaaluma, alisema: “Kabla ya Michezo ya Dunia na Asia, nilijitolea kwa dhati kukabidhi nishani zangu kwenye kituo hiki iwapo zingekuwa dhahabu. Leo, nina heshima ya kutimiza ahadi hiyo kwa kuwasilisha binafsi nishani zangu kwenye kwa Jumba la Makumbusho la Haram Takatifu ya Imam Ridha (AS.”

"Nina mapenzi ya kina na hisia ya kujitolea kwa Imam Ridha (AS) tangu utoto wangu. Niliingia naye katika mpango huu wa kushinda na ninatamani kuendelea kupokea msaada wake katika siku zijazo," aliongeza.

Zare alimalizia kwa kusema: "Siku zote natafuta usikivu na usaidizi wa Imam Ridha (AS) kabla ya mashindano yangu, na ninatumai kwamba wanamichezo wote wa Iran, hususan kizazi kijacho, wataanzisha uhusiano wa dhati na Imam Ridha (AS) pia."

Mwanamieleka huyo mwenye uzito wa kilo 125 alikuwa ameshinda medali za dhahabu katika Michezo ya Asia ya Hangzhou 2022 na Mashindano ya Dunia ya Mieleka ya 2023 mjini Belgrade, Serbia.

3485878

Habari zinazohusiana
captcha