IQNA

Wanamichezo Waislamu

Mchezaji soka wa Ujerumani Robert Bauer akubali Uislamu

21:37 - September 14, 2023
Habari ID: 3477598
BERLIN (IQNA) - Mchezaji soka wa Ujerumani anayecheza nchini Saudi Arabia alitangaza kusilimu kwake.

Robert Bauer alitumia akaunti yake ya Instagram kuweka picha yake akisali na kufichua kwamba ameukumbatia Uislamu kupitia kwa mke wake na familia yake.

Bauer aliandika: "Kwa watu wote wanaonitumia ujumbe leo. Nilikuja Uislamu kupitia kwa mke wangu na familia yake. Imepita miaka mingi na ninawashukuru nyinyi nyote kunisaidia na kunitia moyo katika safari yangu."

Kwa sasa Bauer anachezea klabu ya Al-Tai ya Saudi Arabia, amejiunga na Ligi ya Kulipwa ya Saudia kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Mchezaji huo kandanda wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 28 alicheza mechi yake ya kwanza ya Bundesliga 2 mnamo Oktoba 31, 2014 dhidi ya Fortuna Dusseldorf, akichukua nafasi ya Alfredo Morales. Mechi dhidi ya Dramstadt 98 mnamo Novemba 22, 2015 ilimshuhudia Bauer akifunga bao lake la kwanza kwenye Bundesliga.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alihamia Werder Bremen mnamo Agosti 2016 na akatolewa kwa mkopo kwa FC Nurnberg miaka 2 baadaye. Aliendelea mbele kwa kusaini mkataba wa muda mrefu na Klabu ya Urusi inayoitwa FC Arsenal Tula na akahamishia kambi yake hadi Sint-Truiden, Ubelgiji mnamo Septemba 2021.

Bauer aliiwakilisha Ujerumani kwenye Kombe la Dunia la FIFA la U-20 nchini New Zealand mnamo 2015 na alikuwa sehemu ya kikosi cha Olimpiki ya Majira ya joto ya 2016, ambayo ilishuhudia Ujerumani ikitwaa medali ya fedha.

3485176

captcha