Wakuu wa Msikiti huo wamesema wataendelea kuwapa makazi watu masikini katika mwezi wa Januari wakati wa msimu wa baridi kali. Huduma hiyo imekuwa ikitolewa mwezi uliopita wa Disemba na sasa muhula wake umeongezwa kutokana na hali ya hewa ya baridi kali kuendelea.
Jumuiya ya Afya ya Akili Canada (CMHA) inasema katika mji wa Edmonton, kati ya Disemba 23 na 29 ilipokea simu 820 na Disemba 27 ilipokea simu 163 za misaada ya eneo la kulala kutokana na baridi kali iliyofika kiwango cha -33. Aidha Disemba 28 wakati kiwango cha baridi kali kilifika 135 watu 148 walipiga simu wakiomba msaada.
Hali hiyo ya baridi kali mjini Edmonton inatarajiwa kuendela kwa muda wa wiki mbili hivi na hivyo msikiti wa Al Rashid umeamua kuwasaidia wale wanaohitaji msaada.
Kwa muda wa miaka mitatu sasa Msikiti wa Al Rashid umekuwa ukitoa msaada kwa watu takribani 300 kila siku wakati wa msimu wa baridi.