IQNA

Waziri Mkuu wa Canada apinga sheria inayopiga marufuku Hijabu Quebec

13:33 - December 11, 2021
Habari ID: 3474665
TEHRAN (IQNA)- Ofisi ya Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau imetangaza kuchukua hatua za kisheria dhidi ya sheria ya jimbo la Quebec ambayo imepelekea mwalimu mmoja Muislamu ahamishwe kazi kwa sababu tu alikuwa amevaa Hijabu.

Mwalimu wa darasa la tatu katika eneo la Chelsea jimboni Quebec alihamishwa na kupewa kazi nyingine kwa sababu kwa mujibu wa sheria ya Quebec ambayo inawataka maafisa wa umma kutoonyesha nembo za kidini wakiwa kazini.

Jimbo la Quebec ambalo huzungumza Kifaransa, lilipitisha sheria hiyo mwaka 2019 kwa kisingizio cha kuunga mkono msingi wa usekulari katika sekta ya huduma umma.

Sheria hiyo imelaani vikali kwani inaonekana kuwalenga Waislamu, Makalasinga na Mayahudi.

"Hakuna yeyote anayepaswa kufutwa kazi Canada kutokana na vazi lake au itikadi yake ya kidini," imesema ofisi ya Trudeau katika ujumbe wa baruapepe.

Jumuiya ya Asasi za Uhuru wa Kiraia Canada pamoja na Baraza la Kitaifa la Waislamu Canada zitashirikiana na makundi mengine katika kufikisha kesi mahakamani mwka ujao kupinga sheria hiyo ya Quebec.

Uislamu ni dini inayoenea kwa kasi zaidi Canada ambapo Waislamu wameongezeka kwa asilimia 82 katika kipindi cha muoongo moja uliopita. Hivi sasa Waislamu ni karibu asilimia 3.5 ya watu wote milioni 38 nchini Canada.

Disemba mwaka 2017, Trudeau katika ujumbe wake kwa Kongamano la Kuhuisha Uislamu alisema Waislamu nchini Canada wamekuwa na mchango mkubwa na ni rasilimali muhimu kwa nchi.

"Canada ina bahati kuwa na jamii ya Waislamu wenye harakati," alisema Trudeau katika ujumbe wake maalumu kwa njia ya video.

"Kwa muda wa miaka mingi, Waislamu nchini Canada wameweza kupata ustawi na kutoa mchango mkubwa kwa jamii  huku wakiwa wanadumisha ufungamano muhimu na nchi zao za asili na jambo hilo limewawezesha kuwa na turathi nzuri ya utamaduni."

3476882

Kishikizo: canada hijabu waislamu
captcha