IQNA

Saudia yaruhusu watu laki moja kutekeleza Hija ndogo (Umrah) kwa siku

22:50 - October 01, 2021
Habari ID: 3474369
TEHRAN (IQNA)- Idadi ya Waislamu watakaruhusiwa kutekelelza Hija ndogo au Umrah na kuswali katika Msikiti Mtakatifu wa Makka (Masjid al-Haram) imeongezeka hadi laki moja kwa siku kuanzia Oktoba Mosi.

Hani bin Hosni Haidar, msemaji wa idara ya usimamizi wa Masjid al-Haram anasema wale wote wanaoshiriki katika ibada ya Umrah watalazimika kuzingatia kanuni zote za kiafya za kuzuia maambukizi ya COVID.-19.

Kuanzia Agosti 10 Saudia iliruhusu Waislamu kutoke nje ya ufalme huo kuanza kutekeleza ibada ya Umrah sharti kuwa wawe wamepata chanjo kamili ya COVID-19. Hadi sasa chanjo ambazo zimeidhinishwa na utawala wa Saudia ni zile za  Pfizer-BioNTech, AstraZeneca, Moderna and Johnson & Johnson. Aidha Waislamu kutoka nchi ambazo zimepigwa marufuku kuwa na safari za moja kwa moja kuelekea Saudia watalazimika kuzingatia sheria za karantini watakapowasili katika ufalme huo.

Kama ilivyokuwa mwaka jana na kwa uamuzi uliochukuliwa na serikali ya Saudi Arabia, ibada ya Hija ya mwaka huu pia imefanyika kwa kushirikisha mahujaji elfu sitini tu ambao ni raia wa Saudia na wageni waishio nchini humo kwa sasa.

Uendeshaji wa shughuli za Ibada tukufu za Hija na Umra umewekewa masharti na mipaka nchini Saudia katika hali ambayo, hivi karibuni watumiaji wa mitandao ya kijamii katika nchi hiyo wamelalamikia vikali sherehe za misimu na matamasha ya muziki yanayofanyika nchini humo.

3475857

captcha