Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Qarii Kazem Azar-Pira wa Iran alichukua nafasi ya kwanza katika kategoria ya qiraa ambapo nafasi ya pili ilichukuliwa na mwakilishi wa Uturuki.
Mashindano hayo ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu yalikuwa na washiriki 75 kutoka nchi 42.
Mwaka 2016 pia, mwakilishi wa Iran katika kategoria ya qiraa alishika nafasi ya pili.