IQNA

Wanawake katika mashindano ya Qur’ani Beni, DRC

1:54 - July 19, 2015
Habari ID: 3329125
Mashindano ya Qur’ani Tukufu kwa ajli ya wanawake yamefanyika Ijumaa hii katika Shule ya Kiislamu ya Beni huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mkoani Kivu Kusini.

Nafasi ya kwanza katika mashindano hayo imechukuliwa na Bi. Kismati Hassan mwenye umri wa miaka 23. “Nina furaha kushinda mashindano hayo hasa kwa sababu wanawake wengi kama mimi huwa tu wakijishughulisha na kazi za nyumbani,” ameliambia Shirika la Habari la Anadolu.
Kama mshindi kati ya washiriki 78, Bi. Hassan atapata fursa ya kuenda kuhiji mjini Makka katika safari itakayogharamiwa na Jumuiya ya Kiislamu Kongo COMICO.
Nafasi ya pili katika mashindano hayo imechukuliwa na Kurishidah Rashid mwenye umri wa miaka 41 na ambaye amepata zawadi ya $400 na nakala ya Qur’ani Tukufu.
Mashindano hayo si ya Qur’ani Tukufu tu bali pia washiriki huzingatia ujuzi wa kimsingi kuhusu Fiqhi ya Kiislamu.
Zawadi mbali mbali zilitolewa kwa  washiriki wengine katika mashindnao hayo.
“Zawadi hizi zinakusudia kuwapa motisha wanawake ambao pamoja na kukumbwa na matatizo mengi wanajitahidi pia kujifunza Qur’ani Tukufu,” amesema mwakilishi wa COMICO Imam Sheikh Al Haji Ali Amin.../mh

3329052

captcha