IQNA

Ahul Bayt AS

Kikao cha Usomaji Qur'ani mjini Najaf kabla ya maadhimisho ya kuzaliwa kwa Imam Ali AS

19:05 - January 21, 2024
Habari ID: 3478227
IQNA – Haram Tukufu ya Imam Ali (AS) huko Najaf, Iraq, inaandaa programu ya kimataifa ya usomaji wa Qur'ani Tukufu iliyoanza Jumamosi.

Idara ya Mfawidhi wa Haram hiyo tukufu imeandaa tukio hilo la Qur'ani kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kuzaliwa Imam wa kwanza (AS).

Baadhi ya maqari wakuu wa Iraq pamoja na wasomaji kutoka nchi nyingine, akiwemo Hamid Reza Ahmadivafa kutoka Iran, watasoma Qur'ani Tukufu katika hafla hiyo , Ala Muhsin, mkuu wa Kituo cha Dar-ol-Quran cha Idara ya Mfawidhi wa Haram ya Imam Ali (AS), amesema.

Waislamu wa madhehebu ya Shia na wengineo husherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imam Ali (AS) katika siku ya 13 ya mwezi wa mwandamo wa Rajab, ambayo mwaka huu inaadhimishwa Alhamisi, Januari 25.

Imam Ali (AS) alikuwa mkwe na binamu yake Mtume Muhammad (SAW) na pia Imam wa kwanza katika Uislamu wa Shia.

Imam anaheshimika kwa ujasiri wake, elimu, imani, uaminifu, utiifu usiopinda kwa Uislamu, uaminifu mkubwa kwa Mtume Muhammad (SAW), kuwatendea sawa Waislamu wote na ukarimu wa kuwasamehe maadui zake walioshindwa.

 

 

3486887

Kishikizo: imam ali as
captcha