IQNA

Harakati za Qur'ani

Mashindano ya kuhifadhi na kufasiri Qur'ani nchini Mali

18:43 - January 21, 2024
Habari ID: 3478225
IQNA - Mashindano ya kuhifadhi na kufasiri Qur'ani Tukufu yameanza huko Bamako, mji mkuu wa Mali siku ya Ijumaa.

Jumuiya ya kituo cha kuhifadhi Qur'ani nchini humo imeandaa hafla hiyo kwa ushirikiano na Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya Saudia, kwa mujibu wa tovuti ya Al-Tawasul.

Jumla ya watu 100 wanashindana katika sehemu mbili za mashindano hayo yanayojumuisha wanaume na wanawake.

Kategoria za mashindano hayo ni pamoja na kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu pamoja na tafsiri ya aya,  kuhifadhi nusu ya Qur'ani na kuhifadhi robo ya Qur'ani.

Hafla hiyo imeandaliwa kwa lengo la kutumikia kitabu cha Mwenyezi Mungu, kukuza uhifadhi na uelewa wa tafsiri ya Qur'ani Tukufu na kuwahimiza wahifadhi kuimarisha ujuzi huu wa Qur'ani.

Jamhuri ya Mali ni nchi isiyo na bahari katika Afrika Magharibi. ni nchi ya nane kwa ukubwa barani Afrika. Idadi kubwa ya wakazi wa Mali ni Waislamu.

Kishikizo: qurani tukufu mali
captcha