IQNA

Wanazuoni

Ayatullah Khamenei amtaja Allahmah Tabatabai kuwa shakhsia wa kipekee

11:00 - November 16, 2023
Habari ID: 3477899
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza alipokutana na waandaaji wa Kongamano la Kimataifa la Allamah Tabatabai kuwa: Msingi imara wa kifikra ni hitajio la leo.

Tovuti ya habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu imeripoti kuwa: Nakala ya hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyotoa katika kikao na waandaaji wa Kongamano la Kimataifa la Allamah Tabatabai mnano tarehe 8 mwezi huu wa Novemba  imetolewa na kusomwa leo asubuhi katika ukumbi wa mkutano uliofanyika katika mji wa Qum.   

Katika kikao hicho, Ayatullah Khamenei amemtaja marehemu Allamah Tabatabai kuwa ni shakhsia wa kipekee katika nyanja za kielimu katika karne za karibuni na kusema: Moja ya kazi muhimu za Sayyid Muhammad Hossein Tabatabai mkabala wa uvamizi wa fikra kutoka nje na wa nchi ajinabi ni kuasisi jihadi ya kifikra na msingi madhubuti wa kifikra ambavyo leo tunavihitajia. 

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria sifa adhimu na muhimu zaidi za marehemu Allamah Tabatabai kama elimu, uchamungu, sifa za kimaadili, kipaji cha sanaa, ushairi na fasihi, upendo, urafiki na uamnifu na kuongeza kuwa: Katika upande wa elimu wa Allamah Tabatabai kuna nyuga tofauti, miongoni mwao ni kuwa na anuai za elimu ambazo ni nadra kushuhudiwa.

Ayatullah Khamenei ameashiria namna Allamah Tabatabai alivyokuwa mahiri katika uga wa elimu kama fiqhi, usuli, hisabati, tafsiri ya Qur'ani, elimu za Qur'ani, ushairi na fasihi na akasema: mbali na aina kwa aina za kustaajabisha za elimu alizokuwa nazo Allamah Tabatabai, upeo wake wa kina wa kielimu na kifikra katika elimu mbalimbali ulikuwa wa kuajabiwa pia kiasi kwamba alimu huyo alikuwa mwanausuli mwenye misingi ya kujitegemea, mwanafalsafa mbunifu na mwenye fikra mpya na mfasiri wa Qur'ani wa kuajabiwa.  

Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa: Allamah Tabatabai hivi sasa amejulikana sana ikilinganishwa na wakati wa uhai wake ambapo hakujulikana; na kwa baraka za ikhlasi  yake; shakhsia na athari za Allamah zitazidi kutambulika hapa nchini na duniani kwa ujumla siku baada ya siku. 

 

/4181945

captcha