Baadhi ya nukta hizi kuhusu Khums katika Uislamu ni kama zifuatazo:
Kwa mujibu wa Hadithi, kulipa Khums kutatakasa mali ya mtu na huo ni utangulizi wa kuwa na kizazi kilichotakasika.
Imam Ridha (AS) alisema kwamba Khums ni haki ya Ahl-ul-Bayt (AS), yaani watu wa Nyumba ya Mtume Muhammad (SAW) na ni usaidizi wa njia na mafundisho yao.
Tunasoma katika Hadithi nyingine kwamba Mwislamu wa kweli ni yule ambaye ameshikamana na ahadi yake kwa Mwenyezi Mungu na kwamba mwenye kutamka kwa ulimi wake imani lakini imani hiyo haiku moyoni basi si Mwislamu wa kweli.
Imamu Ridha (AS) alisema Khums ni njia ambayo kwayo tunasaidia jamaa na marafiki zetu.
Imamu Sadiq (AS) alisema kwamba kwa kuchukua dirham kutoka kwa watu (kama Khums), hana nia nyingine zaidi ya kutakasa pesa zao.
Katika Hadith nyingine, Imamu Sadiq (AS) alisema kwamba yeyote anayelipa Khums, mapato yake mengine yatakuwa matamu kwake.
Imam Ridha (AS) alisema kwamba Khums husaidia kulinda sifa ya wafuasi wa Ahl-ul-Bayt (AS.
Imam Kadhim (AS) alisema kwamba Mwenyezi Mungu ameweka nusu ya Khums kwa ajili ya kuwaondolea umasikini kizazi cha Mtukufu Mtume (SAW) ambao hawawezi kunufaika na Zaka na Sadaka.
Imamu Ridha (AS) alisema kwamba kulipa Khums kutoka kwenye pesa za mtu kunasababisha kusamehewa madhambi yake na itakuwa ni hifadhi ya Siku ya Kiyama.
Mtu mmoja alikwenda kwa Imam Baqir (AS) na akalipa Khums zake. Imam (AS) alisema ni muhimu kwani itamdhaminia mtu huyo pepo.
Imamu Ridha (AS) amesema: “Khums inatusaidia katika kuhifadhi itikadi ya (Ahl-ul-Bayt).” Kisha akasema: “Msijaribu kujinyima nafsi zenu na maombi yetu kadri mwezavyo.”
Imam Ridha (AS) alisema: “Kulipa Khums ni ufunguo wa riziki yako.”
Mwenye kuhesabu Khums zake na kuzilipa kila mwaka, ni mtu mwenye utaratibu na nidhamu.
Imam Baqir (AS) amesema: “Ukamilifu wa hali ya juu ni katika mambo matatu: Kuwa na elimu ya kina ya dini, uthabiti katika kukabiliana na matatizo, na kuwa na utaratibu na mipango katika maisha.
Wale wanaolipa Khums hakika watapata usikivu maalum na baraka za Mungu.
Qur'ani Tukufu inasema, “Basi nikumbukeni Mimi, nitakukumbukani”? (Aya ya 152 ya Surah Al-Baqarah)
Qur'ani Tukufu inasema, “Ukifanya wema, itakuwa kwa faida yako mwenyewe”? (Aya ya 7 ya Suratul Israa)
Qur'ani Tukufu inasema: “Na mnapoamkiwa kwa maamkio, basi itikieni kwa yaliyo bora kuliko hayo, au rejesheni. Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuhisabu kila kitu,” (Aya ya 86 ya Surat An-Nisaa)
Qur'ani Tukufu inasema: “Enyi Waumini, kama mkimnusuru Mwenyezi Mungu, atakunusuruni na atakuwekeni imara (katika imani yenu)” (Aya ya 7 ya Surah Muhammad)
Qur'ani Tukufu inasema: “Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wafanyao wema”? (Aya ya 195 ya Surah Al-Baqarah)
Hivyo atakayelipa Khums atajumuishwa miongoni mwa wale ambao aya zilizotajwa hapo juu zinawahusu.