IQNA

Watetezi wa Qur'ani Tukufu

Qur'ani daima itabaki katika nyoyo Za Waislam, hafidha wa Qur'ani awaambia wenye chuki

8:03 - September 28, 2023
Habari ID: 3477661
AMMAN (IQNA) – Hafidha wa Qur'ani Tukufu kutoka Jordan aliyeshinda Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Dubai kwa wanawake anasema Qur'ani Tukkufu itasalia katika mioyo ya Waislamu licha ya vitendo vyote vya kufuru dhidi yake.

Sondos Sidawi, 21, anaona ushindi wake katika mashindano ya kimataifa ya kuhifadhi Qur'ani kama ujumbe wenye nguvu kwa wale wanaofanya vitendo vya kuvunjia heshima Kitabu Hicho Kitukufu.

"Hata wakichoma nakala za Qur'an, itabaki mioyoni mwetu," Sondos ameliambia Shirika la Habari la Anadolu.

Mwanadada huyo alishika nafasi ya  kwanza katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Dubai ya Sheikha Fatima Bint Mubarak kwa wanawake, yaliyofanyika Dubai kuanzia Septemba 16 hadi 22, baada ya kushindana na washiriki 60.

Anatoka katika familia ambayo inajitolea kwa Qur'ani Tukufu kwani ana ndugu watano, watatu kati yao wamehifadhi kikamilifu kitabu hicho kitakatifu.

Sondos "alianza kujifunza Qur'ani Tukufu katika moja ya misikiti katika mji wa Ramtha (kaskazini magharibi mwa Jordan) akiwa na umri wa miaka 11 na kuhifadhi Juzuu 12 katika muda wa chini ya mwaka mmoja, " mjomba wake Saeb Sidawi amesema.

Anasema ilimchukua msichana huyo miezi 22 kuhifadhi kikamilifu aya zote za Qur'ani Tukufu.

"Alitumia masaa mawili kwa siku kuhifadhi Qur'ani Tukufu. Wakati wa likizo, alikuwa akianza alfajiri na kuendelea hadi sala ya jioni," Saeb alisema.

Habari zinazohusiana
Kishikizo: qurani tukufu dihqa
captcha