IQNA

Jinai za Israel

OIC yalaani uvamizi unaoendelea wa Israel dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa

18:57 - August 03, 2023
Habari ID: 3477376
TEHRAN (IQNA) - Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) wamelaani uvamizi wa mara kwa mara wa wanajeshi wa utawala haramu Israel na walowezi wa Kizayuni wenye itikadi kali kwenye jengo la Msikiti wa al-Aqsa mjini Quds (Jerusalem), na kuutaja utaratibu huo kuwa ni uvunjaji wa sheria za kimataifa.

Mwishoni mwa kikao cha 18 kisicho cha kawaida cha Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa OIC huko Jeddah, Saudi Arabia, wanadiplomasia wakuu wamelaani ukiukaji na uchochezi unaoendelea wa utawala haramu Israel katika eneo hilo takatifu kuwa ni "ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa na uhujumu usio na kifani. "na hali ya sasa ya kihistoria na kisheria."

Vile vile walisikitishwa na kitendo cha kudhalilishwa mara kwa mara Msikiti wa al-Aqsa na waziri wa siasa kali za mrengo wa kulia wa Israel Itamar Ben-Gvir, maafisa wengine wa utawala huo na wajumbe wa bunge la Knesset (Bunge) wakieleza kuwa vitendo hivyo ni "vitendo vya uchochezi dhidi ya taifa la Kiislamu."

Siku ya Jumatano, makumi ya walowezi wa Israel walivamia katika eneo la Msikiti wa al-Aqsa chini ya ulinzi mkali kutoka kwa wanajeshi wa Israel.

Walowezi hao wenye msimamo mkali, waliogawanywa katika vikundi, waliingia kwenye tovuti hiyo kupitia Lango la Maghariba na kufanya matambiko na maombi ya Talmudi kwa uchochezi.

Kiwanja cha Msikiti wa al-Aqsa, ambacho kipo juu kidogo ya eneo la Ukuta wa Magharibi, ni nyumba ya Dome of the Rock na Msikiti wa al-Aqsa.

Maafisa wa utawala haramu wa Israel wenye misimamo mikali na walowezi huvamia mara kwa mara eneo la Msikiti wa al-Aqsa katika mji huo unaokaliwa kwa mabavu, hatua ya uchochezi inayowakasirisha Wapalestina. Ukiukaji huo wa Wazayuni dhidi ya Msiktii wa Al Aqsa hufanyika kwa amri ya makundi yenye misimamo mikali yanayoungwa mkono na Tel Aviv na chini ya usimamizi wa polisi wa Israel huko al-Quds.

Mwezi Mei 2021, vitendo vya ukatili vya mara kwa mara dhidi ya waumini wa Kipalestina katika Msikiti wa al-Aqsa vilisababisha vita vya siku 11 kati ya makundi ya muqawama wa Palestina katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa na utawala wa Israel, ambapo jeshi la utawala huo liliua Wapalestina wasiopungua 260 wakiwemo 66. watoto.

3484612

Habari zinazohusiana
captcha