IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Papa Francis vitendo vya kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu

17:06 - July 03, 2023
Habari ID: 3477230
ROME (IQNA) - Papa Francis, Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, amelaani kibali alichopewa mtu mwenye msimamo mkali kuchoma nakala ya Qur'ani Tukufu nchini Uswidi wiki iliyopita.

Akizungumza na gazeti la al-Ittihad la UAE, Papa Francis alisisitiza kuwa kuruhusu kuchomwa moto Qur'ani Tukufu ni kosa la kulaaniwa.

Papa Francis pia alionyesha hasira kali kwa vitendo kama vile kuchoma Qur'ani Tukufu.

Mwanamume wa miaka 37 mwenye asili ya Iraq aliivunjia heshima Qur'ani Tukufu kwa kuchoma baadhi ya kurasa zake nje ya Msikiti Mkuu wa Stockholm siku ya Jumatano. Polisi wa Uswidi waliruhusu na kulinda kitendo cha kutoheshimu kitabu hicho kitakatifu cha Waislamu.

Tukio hilo lililotokea wakati wa Eid al-Adha ya Waislamu na kuhitimishwa kwa ibada ya kila mwaka ya kuhiji Makka huko Saudi Arabia, lililaaniwa vikali na Waislamu duniani kote.

Siku ya Ijumaa, kwa siku ya pili mfululizo, maelfu ya Wairaki walikusanyika karibu na ubalozi wa Uswidi huko Baghdad kushutumu uchomaji wa Quran. Siku moja kabla, waandamanaji wenye hasira walivamia ubalozi huo kwa muda mfupi.

Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) ilifanya mkutano usio wa kawaida siku ya Jumapili, ikisisitiza kwamba sheria za kimataifa zinapaswa kutumika kukomesha chuki za kidini. "Lazima tutume vikumbusho vya mara kwa mara kwa jumuiya ya kimataifa kuhusu matumizi ya haraka ya sheria ya kimataifa, ambayo inakataza wazi utetezi wowote wa chuki ya kidini," Katibu Mkuu wa OIC Hissein Brahim Taha alisema.

4152145

Kishikizo: papa francis uswidi
captcha