IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya 30 ya Kimataifa ya Qur’ani ya Jordan yamalizika kwa washindi kupata zawadi

21:07 - April 18, 2023
Habari ID: 3476886
TEHRAN (IQNA) - Toleo la 30 la Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Jordan yamemefungwa huko Amman Jumatatu usiku.

Sherehe ya kufunga ilifanyika katika Msikiti wa Mfalme Hussein Bin Talal na ambapo maafisa wa ngazi za juu wa Jordan walishiriki akiwemo  Mfalme Abdullah II wa nchi hiyo.

Waandaaji walikabidhi tuzo kwa watu 37 wa Jordan ambao walikuwa wamepata nafasi za juu katika kitengo cha kitaifa cha mashindano na pia kwa watu tisa ambao walishinda katika kitenge cha kimataifa.

Tuzo ya juu ya sehemu ya kimataifa ilipewa Nadi Saad Jaber Muhammad kutoka Misri,  Muhammad Abdul Khaliq Batil kutoka Kanada, Muhammad el Amin Adam Moussa kutoka Chad, Abu Bakr Muhammad Bila Jalo wa Kenya, na Ezzeddin Omar Ahmed Ibrahim kutoka Yemen kwa taratibu hiyo.

 

Sehemu ya wanaume ya mashindano hayo ya Qur’ani ilizinduliwa katika mji mkuu wa Jordan, Amman mnamo Aprili 11. Sehemu ya wanawake ilifanyika mapema mwezi Machi.

Wahifadhi wa Qur’ani wapatao 250 kutoka Jordan na nchi zingine walishiriki katika sehemu ya wanaume.

4134983

captcha